November 14, 2012

KINANA KATIBU MKUU CCM, MCHEMBA NAIBU, MIGIRO MAHUSIANO YA NJE

Abdulrahman Kinana-Katibu Mkuu wa CCM, Taifa.
Mwigulu Nchemba-Naibu Katibu Mkuu (Bara)
Vuai Ali Vuai-Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
Nape Nnauye, abakia katika Nafasi yake ya Katibu wa Itikadi na Uenezi.
Dr. Asha-Rose Migiro- Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Zakia Meghji-Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha.
 Muhamed Seif Khatib, Katibu wa NEC, Oganaizesheni.

LICHA ya aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Abraham Kinana, kusesema hatogombea tena nafasi za vikao vya juu vya CCM kwa kuwa muda wa 25 wa kukitumikia chama hicho kama kiongozi unatosha lakini Kinana ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho kushika nafasi ya Wilson Mkama.

Taarifa kutoka ndani ya CCM zinasema Abraham Kinana ndiye Katibu Mkuu  huku nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara ikichukuliwa na Mwigulu Mchemba, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Katibu wa Uenezi na Itikafi anaendelea Nape Nnauye, Katibu wa Uchumi na Fedha amerejeshwa Zakhia Hamdan Meghji,  Katibu wa Organizesheni ya Mohamed Seif Khatib na Katibu wa Mahusiano na Mambo ya Nje ni Dk. Asha Rose Migiro.

Jana jioni wajumbe wa mkutano Mkuu wa nane wa CCM uliomalizaka mjini Dodoma walimrejesha madarakani Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete kwa kura 2395 sawa na asilimia 99.92 kati ya kura 2397 zilizopigwa.

Aidha wajumbe hao wapatao 2397 waliopiga kura waliwachagua Philip Mangula kuwa Makamu Mwenyekiti Tanzania bara na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar.

Baadhi ya wadau na wanachama wa chama cha Mapinduzi wanapasha kuwa Kinana utakisaidia sana chama akiwa Katibu Mkuu wa CCM na chama kitakuwa katika mstari mzuri.

Pia wamesema kuwa kwake Katibu Mkuu kutamfanya kuyatekeleza na kusimamaia vyema mapendekezo yote aliyokuwa akiyatoa jana kabla ya kufungwa kwa Mkutano huo mkuu.

No comments:

Post a Comment