November 15, 2012

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAZINDUA KINYWAJI KISICHO NA KILEVI ALVARO

Vijana walioshiriki katika uzinduzi wa kinywaji kisichokuwa na kilevi cha Alvaro kinachotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries,wakigonganisha chupa zao kuashiria ishara ya uzinduzi rasmi wa kinywaji hicho hapo jana jijini Da es Salaam.
 Mmoja kati ya vijana akicheza”Break Dance”wakati wa uzinduzi rasmi wa kinywaji kipya kisichokuwa na kilevi cha Alvaro kinachotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries LTD.

*******
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti imezindua kinywaji kipya kisicho na kilevi kinachoitwa Alvaro ambacho kimekuwa kikizalishwa muda mrefu katika nchi nyingine za Afrika Mashariki. Katika uzinduzi wa aina yake uliofanyika mwishoni mwa wiki jijin Dar es Salaam, Meneja wa Kinywaji hicho Anita Msangi alisema kinywaji hicho kitakidhi wateja wanaotumia vinywaji visivyo na kilevi

Uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika katika kumbi za Mlimani City na Quality Plaza jijini, Dar es Salaam, ulivutia watu kutoka matabaka mbalimbali ambao walionekana kufuruhishwa na ladha ya kinywaji hicho. Akizungumza katika sherehe hizo, Bw. Njowoka aliahidi watumiaji wa kinywaji hicho na vingine vinavyotengezwa na kampuni ya Serengeti kuwa kampuni yake imejipanga kuona kuwa wateja wanapata bidhaa bora zenye viwango vya hali ya juu vinavyostahili na kukidhi matakwa ya wateja wake.

Pamoja na wageni wengi waliofika kwenye uzinduzi huo, sherehe za kuzindua kinywaji hicho pia zilipambwa na vikundi mbalimbali vya vijana ambavyo vilionesha uweso mkubwa katika sanaa ya muziki pamoja na kucheza dansi. Kinywaji cha Alvaro kimekua kikizalishwa kwa muda mrefu katika nchi za Uganda na Kenya kupitia kampuni mama ya kiwanda cha kutengzeneza bia cha Serengeti iitwayo East African Breweries Limited.

No comments:

Post a Comment