Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) na Balozi wa Airttel Tanzania, Ambwene Yessaya 'AY'
Afisa
Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na Msanii wa muziki wa kizazi kipya
(Bongo flava) kwa pamoja wakionyesha tuzo ya Channel O aliyoipata
Mwanamuzi huyo nchini Afrika Kusini. Tukio hilo limefanyika leo wakati
wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Airtel imempongeza AY kwa
ushindi alioupa pamoja na kumwandalia sherehe ya kumpongeza
itakayofanyika leo usiku nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) na Balozi wa Ambwene Yessaya
'AY' akiwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kumwezesha kupata tuzo
hiyo kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na kushoto ni DJ
wake Athur Baraka.
Afisa
Uhusiano wa Airtel Jane Matinde akiongea wakati wa mkutano na waandishi
wa habari ambapo Airtel imempongeza AY balozi wake kwa kupata tuzo ya
chanel O ya video bora, Katikati ni AY akifatiwa na DJ wake Athur
Baraka
******
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel wakiwa na balozi wake Ambwene Yessaya “AY”
leo wamewashukuru watanzania kwa kumpigia kura msaani maarufu wa kizazi
kipya Ambwene Yessaya “ AY “ na kumwezesha kuibuka mshindi wa tuzo ya kwanza katika kipengele cha Most Gifted East African video of the Year kupitia kibao chake kipya kijulikanacho kama “ I don’t wanna be alone”
Akiongea
na wandishi wa habari katika Ofisi za Airtel leo AY amechukua fulsa
kuwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kuweza kumwezesha kuibuka na
ushindi. Aidha alivishukuru vyombo vya habari kwa kuendelea
kushirikiana naye katika kufikisha habari na kumsaidia kupata tuzo hiyo.
Naye
Afisa uhusino wa Airtel Jane Matinde alisema” tunafurahi kuona msanii
AY ambaye ni balozi wetu kuibuka na tuzo iliyoshirikisha wasanii
mbalimbali toka Afrika, sisi tunasikia furaha kuona mafanikio ya
wasanii wetu nchini yakiendelea kukua na ndio sababu leo tuko hapa
kusherehekea ushindi huu kwa pamoja na kuwashukuru watanzania kwa
kumuwezesha AY kupata tuzo hii kwa kura zenu.
Tunapenda
pia kuchukua fulsa hii kuwaalika watanzani na wateja wetu leo pale
nyumbani lounge usiku kuanzi saa tatu tuweze kujumuika na AY na
kumpongeza kupata tuzo hii. Tutakuwa na wasanii wengi pamoja na wadau
mbalimbali wa Musiki na pia utapata muda kupiga picha na msanii huyo na
Tuzo yake.
No comments:
Post a Comment