Warembo wa wanaoshiriki shindano la kumsakama Malkia wa Tabata 2012 wakipozi mbele ya mashabiki wa burudani ya urembo jijini Dar es Salaam waliohudhuria uzinduzi wa shindano hilo la Urembo katika Ukumbi wa Dar West Park Tabata jana.
Warembo wakicheza Show maalum ya utambulisho wao. Goma la Don’t Take My Number ndo liliwaongoza.
Warembo wa wanaoshiriki shindano la kumsakama Malkia wa Tabata 2012 wakipozi mbele ya mashabiki wa burudani ya urembo jijini Dar es Salaam waliohudhuria uzinduzi wa shindano hilo la Urembo katika Ukumbi wa Dar West Park Tabata jana.
Washiriki wa Shindano la Miss Ukonga 2012 ndio waliowasindikiza majirani zao wa Tabata.
Mpiga drams wa Twanga Pepeta Martin Kibosho akifanya vitu vyake jukwaani.
Mwimbaji mkongwe asiyechoka wala kuzeeka, Mumin Mwijuma akikamua na kundi lake la Twanga Pepeta.
Wanenguaji wa Bendi ya Twanga Pepeta wakishambulia Jukwaa vilivyo.
Shabiki mkubwa wa Twanga, Tomm Chilala akiyarudi magoma na mdau mwenzake.
Ilikuwa ni mshike Mshike kwa show za kufa mtu hakuna kukaa.
Wadau wa Burudani na Urembo wakifatilia burudani na uzinduzi ho ulioletwa na Bob Interteinment na kudhaminiwa na Konyagi na Dodoma Wine.
Mzee Mzima Salum Simba (MC) machachari akiwa na my wife wake.
Wadau wakubwa wa masuala ya urembo na Burudani kwa ujumla walikuwepo ukumbini. Pia walitumia fursa hiyo kusheherekea Pasaka.
Jopo la waandaaaji wa Shindano la Miss Chan'gombe walikuwepo kuangalia vitisho vya Miss Tabata 2011. Kushoto ni Mmoja wa washiriki wa Miss Chang'ombe ambaye hakika ni fimbo ya ukweli.
Mwana dada Aisha Ramadhani "Aisha Mashauzi" aliwashika vilivyo na walikatika nyonga ile mbaya kwa taarabu yake kali.
Wadau mbalimbali wa Burudani na Urembo walihudhuria katika uzinduzi huo ulioenda sambamba na Show kali kutoka kwao Twanga Pepeta “Kisima cha Burudani” na Mashauzi Clasic Modern Taarab kutoka kwake Mtoto wa Kikurya Aisha Ramadhani ‘Mashauzi’.
No comments:
Post a Comment