April 10, 2012

Safari ya Mwisho ya Steven Kanumba

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu,Steven Kanumba likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam asubuhi hii

Mama mmoja alijikuta akianguka na kukosa nguvu ghafla kufuatia uchungu mkubwa wa kifo cha mpendwa wao Steven kanumba.
Hongereni sasa wafanyakazi wa chama cha Msalaba Mwekundu,kwa hiki mlichokifanya hapa lidaz Club,Mungu awape nguvu,imani na upendo kwa wakati huu mgumu tulionao sasa.
Viongozi mbalimbali wa Kiserikali wakiwepo kuaga mwili wa Steven kanumba mapema leo
Wa Pili kulia ni Mama yake na Marehemu Steven Kanumba akiwa ameambatana ndugu jamaa na marafiki kumuaga mtoto wao kabla ya kwenda kulazwa kwenye nyumba yake ya milele jioni ya leo.
Kikundi cha kwaya kikiimba mbele ya umati mkubwa wa watu uliofika kwenye viwanja hivi kumuaga mpendwa wao. 
Umati wa watu uliojitokeza Kuaga mwili wa marehemu steven Kanumba katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, sasa watu ni wengi hadi imeshindikana kuaaga jambo ambalo limepelekea watu kuzimia hovyo hasa akina dada,huku kikubdi cha huduma ya kwanza kutoka Red Cross kikifanya kazi yake ipasavyo kuwasaidia watu mbalimbali waliokuwa wakikubwa na tatizo la aina yoyote.  
 Mama wa marehemu akiwa ameongozana na ndugu jamaa na marafiki wakiwasili.
 
Rais wa chama cha Wasanii wa Filamu nchini,Saimon Mwakifwamba akisoma hotuba fupi iliyohusu mambo mbalimbali kuhusiana na msiba huo mkubwa wa kuondokewa na Mpendwa wetu,Steven Kanumba.
Wapigaji wenzangu nao wako bize kuchukua matukio mbalimbali ya kumbukumbu.
Watu wengi walizimia kama uonavyo pichani,hasa wanawake ambao kiukweli walikuwa na hisia sana juu ya msiba huu.  
Utaratibu ukiwekwa sawa kwa ajili ya kumuaga marehemu Steven kanumba.
Baadhi ya watoto wa Rais Kikwete,wakiwasili tayari kwa kumuaga mpendwa wao,rafiki yao. 
Gari iliyokuwa imebeba mwili wa Marehemu Steven Kanumba ukiwasili kwenye viwanja vya Lidaz Club leo asubuhi tayari kwa kuagwa.
Umati mkubwa wa watu ukiwa nje ya viwanja vya lidaz mapema leo asubuhi wakati wa kuaga mwili wa marehemu,Steven kanumba.

1 comment:

  1. inauma kweli jamani tumempoteza mpendwa wetu kipenzi chetu.

    ReplyDelete