Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk Ali Muhammed Shein leo amewabadilisha baadhi ya mawaziri katika baadhi ya wizara.
Kwa mijibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu wa Baraza la Mapinduzi na katimbu mkuuu kiongozi dk Abdulhamid Yahya Mzee mawaziri waliobadilishwa Wizara ni pamoja na
Ramadhani Abdalla Shaaban ambaye sasa anakuwa Waziri wa Ardhi, Makaazi Maji na Nishati na Ali Juma Shamuhuna anakuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali..
Kabla ya mabadiliko hayo Ramadhani Abdalla Shaaban alikuwa ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wakati Ali Juma Shamuhuna alikuwa Waziri wa Ardhi, Makaazi Maji na Nishati.
Wengine waliobadilishwa wizara ni Mansour Yussuf Himid ambaye sasa anakuwa Mjumbe wa baraza la mapinduzi na Waziri asiyekuwa na Wizara maalum. Wakati Suleiman Othman Nyanga anakuwa waziri wa Kilimo na Maliasili.
Kabla ya mabadiliko hayo Mansour alikuwa ni Waziri wa kilimo na maliasili wakati mhe. Suleiman othman nyanga alikuwa mjumbe wa baraza la mapinduzi na waziri asiyekuwa na wizara maalum.
Taarifa hiyo ya katibu wa baraza la mapinduzi na katibu mkuu kiongozi pia imeeleza kuwa Abdillah Jihad Hassan anakuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi wakati Said Ali Mbarouk ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo.
Kabla ya mabadiliko hayo Abdillah jihadi hassan alikuwa ni Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo na Said alikuwa ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
Aidha Rais Shein amemteua Sheha Muhammed Sheha kuwa mshauri wa Rais Pemba.
No comments:
Post a Comment