April 11, 2012

MKOA WA RUKWA WAJIPANGA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WOTE WALIOFAULU KWENDA KIDATO CHA KWANZA WANAKWENDA SHULE IFIKAPO april 15

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na viongozi wa kata ya Katandala (Hawako Pichani) katika Ofisi za Kata hiyo katika Manispaa ya Sumbawanga jana kwenye kikao cha Kamati ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Kilimani Azimio ili kuwezesha wanafunzi waliofaulu na kukosa vyumba vya madarasa waweze kwenda Shule kabla ya mwezi huu wa Aprili kuisha. (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)- rukwareview.blogspot.com  

Muamko wa Wananchi wa Mkoa wa Rukwa katika kuchangia kwenye sekta ya elimu umekuwa mdogo jambo lililoilazimu Serikali ya Mkoa kuunda Vikosi kazi viwili kimoja kikiongozwa na Mkuu huyo wa Mkoa na kingine kikiongozwa na Katibu Tawala Mkoa Alhaj Salum Mohammed Chima kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa wananchi katika miradi hiyo ya elimu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Ndugu William Shimwela. (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)  
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na waandishi wa habari Peti Siyame (Dailynews/ Habari Leo, kushoto) na Mussa Mwangoka (Mwananchi, kulia) jana walipotaka kujua juu ya kampeni iliyoanzishwa na Serikali ya Mkoa wa huo katika kuhamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za Sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga ili kuhakikisha wanafunzi waliofaulu wanakwenda shule kabla ya mwezi huu kuisha. Katikati ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Ndugu William Shimwela. Tangu kampeni hiyo ianzishwe ni wiki moja sasa na tayari wananchi wengi wamehamasika kuchangia. (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa) .
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na wakazi wa Kata ya Majengo katika Manispaa ya Sumbawanga huku akiwasisitiza juu ya usafi wa mazingira katika mtaa wao pamoja na kuwaagiza kuchangia katika sekta ya elimu kwa ajili ya ujenzi wa Shule za Kata kama ilivyo sera kuu ya Serikali katika Shule hizo kuwa ni shule za jamii hivyo wanapaswa kuchangia na Serikali kuwaongezea nguvu. (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)- rukwareview.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment