April 05, 2012

MBOWE: Jumamosi tutajua kama tutarudia Uchaguzi au kukata Rufaa

Mwenyekiti wa CHADEMA Freman Mbowe (katikati)  akitoa hotuba yake kwa wananchi jijini Arusha leo. Kushoto ni Mbunge mteule  wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nasari na kulia ni  Godbless Lema aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini mara baada ya hukumu kutolewa.
********
MWENYEKITI wa CHADEMA taifa, amewataka wananchi wa Mji wa Arusha kuwa watulivu wakati Chama kinatafakari jambo gani kufanya kati ya kukata rufaa au kurudia uchaguzi huo wa Jimbo la Arusha mjini baada ya Mahakama Kuu kanda ya Arusha kutengua Ubunge wa Mbunge wa Arusha, Godbless Lema hii leo.

Mboye ameyasema hay oleo wakatio akihutubia maelfu ya wakazi wa arusha waliokusanyika katika Ofisi za Chama hicho kujua hatma ya Mbunge wao Godbless Lema ambaye Mahakama imemuondoa madarakini.

Kutokana na hali hiyo Bw Mbowe alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa watulivu kwa kuwa hata chama hicho bado hakina nguvu ya kupingana na nguvu ya mahakama kwa kuwa mahakama ni muhimili pekee wa nguvu ya Dola.

Awali Aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo la Arusha Mjini Goodbless Lema,aliwaambia maelfu ya wananchi ambao walikusanyika katika  viwanja vya mahakama hiyo kuwa bado yeye ni jasiri wa hali ya juu sana na kwa hali hiyo atashinda tu.

Lema alisema kuwa kitu kilichofanyika katika mahakama hiyo na kisha kutengua ubunge wake kiinaonesha wazi jinsi mahakama isivyoweza kutumia demokrasia na hali hiyo kama itaendelea ni wazi kuwa maskini watakosa haki zake za msingi.

HUKUMU
MAHAKAMA Kuu Kanda ya arusha leo imemvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tiketi ya CHADEMA.

Taarifa kutoka jijini Arusha zinasema uamuzi huo umefikiwa leo asubuhi Aprili 5, 2012 mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha hilo yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo.

Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).

Lema katika Uchaguzi huo alikuwa akichuana vikali na Mgombea wa CCM, Dk. Batilda Salha Buruiani ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya.

Akisomewa hukumu hiyo  mapema leo na jaji mfawidhi kutoka katika kanda ya sumbawanga Jaji Gabriel Rwakabirira alisema kuwa ameridhika na ushahidi wa pande zote mbili na ndio maana ametoa hukumu Jaji Gabriel alisema kuwa alipokea dondoo 10 kutoka kwa wafuasi wa CCM ambapo alifanikiwa kuku ali dondoo 8 na kisha kukutaa dondoo nyingine mbili kwa mujibu wa sheria na taratibu za mahakama.

Alisema kuwa Mbunge Lema alitenda makosa hayo kati ya mikutano 60 ambayo aliifanya katika enzi za kampeni za mwaka 2010 ambapo alimchafua Mgombea Mwenza ambaye ni Dkt Batilda Burian kinyume cha sheria Jaji huyo alifafanua kuwa mbunge huyo alikutwa na makosa nane hali ambayo inamfanya mpaka sasa angatuke kwenye ubunge kwa mujibu wa sheria na taratibu za mahakama.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa anamuagiza msajili wa mahakama kwa kanda ya Arusha kuhakikisha kuwa anapeleka taarifa kwa tume ya uchaguzi juu ya kuenguliwa kwa Mbunge huyo lakini bado yuko huru kukata rufaa hata kwa ngazi za juu sana.

Wanachama hao wanadai kuwa taratibu za maadili ya uchaguzi zilikiukwa  wa kuwa mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli katika mikutano ya kampeni aliyofanya jimboni Arusha.

Katika kesi hiyo wadai walileta mashahidi 14 kwenda kutoa ushahidi wao katika mahakama hiyo nawadaiwa walifanikiwa kuwaleta mashahidi 5 kujitetea.

Kuvuliwa Ubunge kwa Lema, kuna kuja siku chache wakati bado cham hicho kipo katika shamra shamra za ushindi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki mkoani humo.
 
Father Kidevu Blog itaendelea kukupa habari zaidi za Hukumu hiyo. 

No comments:

Post a Comment