Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam leo kuhusu Sherehe za Tuzo za Kilimanjaro Music 2012 zitakazofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, siku ya jumamosi wiki ijayo.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) leo wametangaza rasmi tarehe ya usiku wa kutoa Tuzo za Muziki Tanzania (Kilimanjaro Tanzania Music Awards).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Bwana George Kavishe alisema tarehe ya usiku wa kutoa tuzo hizo kuwa ni tarehe 14.Aprili.2012 ndani ya ukumbi wa Mlimani City. “Shughuli itaanza rasmi saa moja jioni ikipambwa na burudani safi iliopangwa kwa umahiri na utaalam kutoka hapa nyumbani. Wasanii watakao pamba usiku wa utoaji tunzo ni pamoja na Diamond, kundi zima la TMK Wanaume, Diamond, Charles Baba, Khalid Chokoraa, Recho, Ommy Dimples, Bichuka na wengine wengii”
Aliendelea Bwana George Kavishe kwa kusema show itakuwa kali kwani sio tu wataimba nyimbo zao lakini wataimba na nyimbo za zamani zilizowahi kutamba za kwao wenye pamoja na wanamuziki nguli nchini.
Meneja huyo wa bia alitoa shukurani kwa Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kupiga kura “ tumevuka lengo la idadi ya kura kwa Nyanja zote ikiwa ni maana ya ujumbe mfupi, vipeperushi, barua pepe, na mitandao , hii inamaanisha Tuzo zimekubalika na zimepokelewa vizuri na jamii”
George pia aliishukuru BASATA kwa kuendelea kutoa ushirikiano na bia ya Kilimanjaro na kuipatia tena kibali cha kudhamini na kuendesha shughuli za Tunzo za Muziki Tanzania.
Taarifa muhimu za usiku wa utoaji tunzo:
Ticket zitauzwa kwa utaratibu ufuatao, VIP 75,000 ikijumuisha chakula cha jioni (buffet) na vinywaji bure na kawaida kwa TSh.20,000 na bia moja ya bure. Maeneo yatakayouza ticket ni:-
1. Ukumbi wa Mlimani city kuanzia jumatatu,
2. Posta - Baraka Garden mtaa wa Azikiwe nyuma ya CRDB Bank.
3. Zizzou Fashion ya Victoria, Sinza na Tegeta.
4. Bornie to Shine Mwenge
5. Robbie One Fashion – Kinondoni
6. Engine Petrol Station – Mbezi.
Waandishi wa habari watapewa vibali maalum vya kuingilia na wale waandishi wapiga picha watakuwa na sehemu maalum ya kufanyia kazi zao. Vitambulisho vya kudhibitisha kuwa ni mwandishi havita tumika usiku huo. Taarifa zaidi watapewa na kampuni ya 1Plus.
No comments:
Post a Comment