April 10, 2012

Maelfu ya Watanzania wamzika Kanumba Dar es Salaam leo.

Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa akiuaga mwili wa mwanaye kwa mara ya mwisho kabla ya kuzikwa rasmi katika makaburi ya Kinondoni.
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa na ndugu wa karibu wakiaga mwili wa marehemu kwa mara ya mwisho makaburini Kinondoni.
 Waombolezaji wakitayarisha jeneza la marehemu Steven Kanumba tayari kwa kuliweka kaburini.
 Mmoja wa waombolezaji akibebwa baada ya kupoteza fahamu makaburini.
 Wajenzi wa kaburi la marehemu wakichanganya Sementi kwa ajili ya kufukia.

 Maqma wa Marehemu Steven Kanumba akiweka shada la maua mkaburini
 Wafanyakazi wa msalaba mwekundu wamefanya kazi ya ziada kutoa huduma ya kwanza kwa waombolezaji
 Maskari wa kusimamia usalama wakiweka uzio kwa ajili ya kuhakikiosha usalama katika mazishi hayo.
 Polisi wakiweka ulizi wa kutosha katika mazishi hayo.
 Kamanda wa Kanda Maalum ya kipolisi mkoa wa Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waombolezaji makaburini Kinondoni.
 Umati huu wote uko makaburini na wengine kama unavyoona wamepanda kwenye miti ili mradi tu waone mazishi ya mpendwa wao Steven Kanumba.
Mwanamitindo maarufu mtanzania anayefanya kazi zake za mitindo nchini Marekani Millen Magese akienda kuweka shada la Maua kwenye kaburi la marehemu Steven Kanumba.

  Makamu wa Rais akimfariji mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa, wakati alipokwenda kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu mwigizaji huyo aliyefanya vizuri sana katika tasnia ya filamu nchini Tanzania na nje ya Tanzania.
 Waigizaji mbalimbali wakiwa katika msiba huo kwenye viwanja vya Leaders leo.
 Rais wa shirikisho la filamu Nchini Bw. Saimon Mwakifwamba akimfariji mmoja wa waombolezaji katika msiba huo.
 Mmoja wa waombolezaji akibebwa juu juu baada ya kuzirai katikamsiba huo.
 Huyu naye hakujiweza ilibidi asaidiwe na wafanyakazi wa Msalaba mwekundu.
 Huyu muombolezaji naye alidondoka baada ya kupoteza fahamu na kuzirai katika viwanja vya Leaders.

 Watoto waliowahi kuigiza na marehemu Steven Kanumba na ambao aliibua vipaji vyao yeye mwenyewe wakiwa wamebea picha ya Marehemu Kanumba.
 Hali ilikuwa ni ya majonzi na waombolezaji wengi walidondoka chini na kupoteza fahamu kutokana na simanzi.
 Viongozi mbalimbali wamehudhuria katika kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadik, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernald Membe, Waziri wa Ardhi na Makazi Prof. Anna Tibaijuka na Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh. Idd Azzan.

Mtangazaji wa Clods TV Regina Mwalekwa akiwajibika katika tukio hilo la kihistoria kwenye viwanja vya Leaders.

3 comments:

  1. RIP Kanumba Kha! kaka watu wengi wametaka kukuona. Natamani ingekuwa movie ufufuke

    ReplyDelete
  2. wapi Ramsey Noah???

    ReplyDelete
  3. mungu aipokee roho yako. amen

    ReplyDelete