Meneja kampeni ya Yanga SMS loyalty kampeni iliyoandaliwa na kampuni ya Push Mobile, Talib Rashid na Mkuu wa Idara ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Kompyuta wa klabu ya Yanga, Baraka Kizuguto wakionyesha zawadi ya jezi ambazo zitatolea kwa mashabiki mbali mbali watakaoshiriki katika bahati nasibu hiyo jana katika uzinduzi wa zoezi hilo jana Makao Makuu ya klabu ya Yanga.
********
Mabingwa wa soka wa Tanzania Bara, Yanga nayo imeingia katika bahati nasibu ya Kampuni ya Push Mobile ambapo mashabiki wake watazawadiwa pikipiki aina ya bajaji yenye thamaniya sh. Milioni 6.
Juzi, kampuni ya Push Mobile ilizindua bahati nasibu hiyo kwa upande wa klabu ya Simba, hata hivyo kampeni meneja wa kampuni hiyo, Talib Rashidi alisema kuwa wameamua kupanua wigo wa kampeni hiyo na kuingia makubaliano ya klabu ya Yanga.
Rashid alisema kuwa Tanzania kwa sasa ina timu kubwa mbili, Yanga na Simba na kuingia mkataba na klabu moja isingekuwa haki kwa mashabiki wa soka hasa wa Yanga ambao ina jumla ya mashabiki zaidi ya 20,000.
Alisema kuwa kama ilivyokuwa kwa mashabiki wa Simba, mashabiki wa Yanga wanatakiwa kutuma ujumbe wa neon Yanga kwenda namba 15678 ili kujiunga katika droo hiyo na kuanza kujibu maswali mbali mbali yahusiyo klabu hiyo kabla ya kupewa kushinda.
“Kuna zawadi nyingi, lakini zawadi kubwa ni pikipiki aina ya bajaji yenye thamani ya shs Milioni, pia kuna pikipiki mbili zenye thamani ya shs milioni 1.5 kila moja, fedha taslimu shs 50,000 kwa washindi wa kila siku na zawadi ya jezi za klabu hiyo,” alisema Talib.
Alisema kuwa bahati nasibu hiyo itadumu kwa siku 90 na kuwataka mashabiki wa Yanga kushiriki kwa ili kupata fursa ya kushinda.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Teknolojia ya Kompyuta wa Yanga, Baraka Kizuguto aliipongeza kampuni ya Push Mobile kwa kuingia nao makubaliano hayo na bahati nasibu hiyo itawawezesha mashabiki wa Yanga kujua mambo mbali mbali ya klabu yao kwa njia ya maswali.
Kizuguto alisema kuwa Yanga kwa sasa ipo katika zoezi la kuboresha takwimu ya wanachama na mashabiki wao ili kujua idadi kamili.
“Bahati Nasibu hii itatuwezesha kujua hatua idadi ya mashabiki wa klabu yetu na ninawaomba wafike kwa wingi, hii ni fursa pekee ya kujishindia zawadi mbali mbali,” alisema Kizuguto.
No comments:
Post a Comment