April 05, 2012

HABARI YA HIVI PUNDE: Godbless Lema avuliwa Ubunge Arusha Mjini

MAHAKAMA Kuu Kanda ya arusha leo imemvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tiketi ya CHADEMA.

Taarifa kutoka jijini Arusha zinasema uamuzi huo umefikiwa leo asubuhi Aprili 5, 2012 mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha hilo yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo. 


Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).


Lema katika Uchaguzi huo alikuwa akichuana vikali na Mgombea wa CCM, Dk. Batilda Salha Buruiani ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya.

Kuvuliwa Ubunge kwa Lema, kuna kuja siku chache wakati bado cham hicho kipo katika shamra shamra za ushindi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki mkoani humo.

Pia habari za ndani ya Chama cha Chadema zinasema kuwa tayari Chama hicho kilisha soma alama za nyakati mapema katika kesi hiyo miezi kadhaa nyuma na kujipanga endapo mbunge huyo atavuliwa wadhifa wake nani kimsimamishe kutetea kiti hicho.

Habari hizo zinadai kuwa Chadema kimepanga kumsimamisha Katibu Mkuu wa Chama hicho na Mgombea Urais wa 2010, Dk. Wilbroad Silaa kutetea kiti hicho.



Wanachama hao wanadai kuwa taratibu za maadili ya uchaguzi zilikiukwa  wa kuwa mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli katika mikutano ya kampeni aliyofanya jimboni Arusha.

Katika kesi hiyo wadai walileta mashahidi 14 kwenda kutoa ushahidi wao katika mahakama hiyo nawadaiwa walifanikiwa kuwaleta mashahidi 5 kujitetea.

Father Kidevu Blog itaendelea kukupa habari zaidi za Hukumu hiyo. 

7 comments:

  1. Mafisadi wamemuandama Lema had kavuliwa ubunge,lakini najua tutajipanga kuchukua tena hilo jimbo, mafsad washindwe!

    ReplyDelete
  2. Hawa watu ni washenzi!! KWan wao hawatukanagi?? Imefanywa haraka sbb wameona wameshapoteza raman, yaani imekula kwao mfa maji haachi kutapa tapa!!! CCM hata mkijipanga mmeshaharibu!! Mnavuta shuka wkt ce tushaamka!!

    ReplyDelete
  3. Nilikuwa najiuliza hivi ni kwa nini CCM walikubali matokeo ya Arumeru Faster Faster.

    Sasa Nimeelewa Mkakati uliowekwa!

    ReplyDelete
  4. hawa jamaa wana hasira imewauma ya Arumeru so wanataka watumie nguvu zooooote ili waipate Arusha mjini, lakini poa 2 jitose mzee mwenyewe afu 2one itakuwaje, wanataka hata itokee vurugu afu wasingizie chadema chama cha vurugu, msajiri akifute. zambi zenu zitawafuata za wizi uliokubuhu.Na nyie CCM hamtataka kuachia ngazi hivi hivi mnatamani muache madaraka nchi ikiwa imechafuka, sasa huo sio uungwana.Miaka 50 bado mnataka kuongezewa muda mpaka lini? ushauri wangu mimi nisiye msomi embu tuwapatie vijana japo ka mwaka kamoja wakichemka sisi tutarudi kwenu, ila kama hamtaki POA 2 TUINGIE ULINGONI 2ONE.

    ReplyDelete
  5. Mapambambano bado yataendelea hata kama wanadhoofisha nguvu za wapambanaji inabidi ijulikane kwamba saa ya ukombozi imefika hakuna kulala mpkaa ukombozi wa kweli utimie

    ReplyDelete
  6. KWAKWELI SIJUWI NNCHI HII INAELEKEA WAPI BADALA YAKUWAZA JINSI YAKUNYANYUWA UCHUMI WA NNCHI WANAWAZA KURUDIA UCHANGUZI NA NI SHILING NGAPI WATAKAZO ZIPOTEZA KWANINI WASIWEKEZE HATA KWENYE MIRADI?UMEME SHIDA MAJI SHIDA NABADO MADENUI KIBAO YA NNCHI YETU JAMANI DAH INACHOSHAAAA?SASA KWA AIBU MUITAFUTAYO CCM MNAZIDI KUJICHAFUWA BADALA YAKUJIOSHAAA?NAAMINI TUTASHINDA KWAKISHINDO PEOPLESSSSS POWER IN GOD WE TRUST?

    ReplyDelete
  7. NAAMINI HILO NA KULIUNGA MKONO NA MM KAMA MM MTANZANIA ALISI LAZIMA NTASIMAMIA HAKI YANGU NA YA NNCHI YANGUUU?PEOPLESSSS POWER

    ReplyDelete