April 12, 2012

Airtel yakabidhi milioni 30 Kwa mshindi wa nani Mkali.

Mshindi wa pili wa milioni thelathini wa promosheni ya  Nani Mkali bwana Steven Chapile kutoka Arusha  akikabidhiwa kitita hicho na Afisa uhusiano wa Airtel Dangio Kaniki mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi
wa pili wa mwenzi wa promosheni ya Nani Mkali  inayoendelea na kuwapa nafasi wateja wa Airtel kujishindia pesa taslimu.
Afisa  uhusiano wa Airtel Bi Dangio Kaniki akikabithi kitita cha shilingi milioni moja kwa Edward Mnewa baada ya kuibuka kuwa mshinidi wa siku na  kujishindia shilling milioni moja  katika promosheni Nani Mkali inayoendelea na kuwapatia wateja wa Airtel nafasi ya kuibuka kuwa washindi.
Afisa  uhusiano wa Airtel Bi Dangio Kaniki akikabithi kitita cha shilingi milioni moja  kwa Camill  Mayo baada ya kuibuka kuwa mshinidi wa siku na kujishindia shilling milioni moja  katika promosheni Nani Mkali inayoendelea na kuwapatia wateja wa Airtel nafasi ya kuibuka kuwa washindi.

********
  •  Wateja wa Airtel kuendelea kujishindia mamilioni
  •  Airtel yazawadia zaidi ya milioni 117 bado milioni 100 kushindaniwa
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imemtanga na kumzawadia mshindi wa pili wa million 30  wa promoshenii ya Nani Mkali bwana Steven A Chapile  ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa  Arusha baada 
ya kuibuka kuwa mshindi wa droo ya mwenzi na kuzawadia kitita cha shilingi milioni 30 katika halfa fupi iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Morocco leo.

Kwa mara nyingine Airtel kupitia promosheni ya Nani Mkali inaendelea kuzawadia wateja wake na kuwawezesha watanzania kujishindia mamilioni ya fedha taslimu, mpaka sasa  zaidi ya shillingi milioni 117 zimeshazawadia kwa wateja wanaoshiriki na Kushinda na bado zaidi ya shilingi million 100 zipo kwaajili ya kuwazawadia wateja watakaoendelea kushiriki katika promosheni hii ya Nani Mkali.

Katika promosheni hii ya Airtel Nani Mkali  washindi wa siku wanazawadia shilingi million 1, washindi wa wiki shilingi milioni 3 na wa mwenzi shilingi  miliioni 30, mbali na kumtangaza mshindi wa shilingi Milioni 30, Airtel pia imewatangaza na kuwazawadia shilingi milioni moja kwa washindi 6 wa wiki ambao ni bwana Yunus Lugendo ambaye ni fundi umeme na mkazi wa babati, Jofrey Shangalawe mfanyakazi wa Tanesco na mkazi wa Shinyanga, David Samson Njole wa  Mbeya, Denis Mugala  ambaye ni mtumishi wa umma na mkazi wa Rukwa, Edgar Mnewa na Camil Mayo wote ni wafanyabiashara na wakazi wa Dar es salaam.

Promosheni hii bado inaendelea kujiunga na "Nani Mkali", mteja anatakiwa kuandika neno "Mkali" na kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi.

No comments:

Post a Comment