January 08, 2012

Azania Bank Tawi la Mbauda Arusha wawazawadia washindi wa ASPIRE ACCOUNT

 Mshindi wa Tatu Kirigiti Chacha Wambura akikabidhiwa hundi yenye thamani ya sh. 1.5 (kulia), akikabidhiwa hundi hiyo na Msaidizi wa Meneja wa benki hiyo Hashim Ally Simchimbey.

 Bank ya azania Jijini Arusha   Tawi la Mbauda imekabidhi zawadi kwa washindi wa ASPIRE ACCOUNT ikiwa ni awamu ya pili, shindano hilo lilishirikisha  wanafunzi wa chuo cha INSITUTE OF ACCOUNTS ARUSHA (IAA).

Shindano hilo ni maalumu kwa wanafunzi ambao bank hiyo imeamua kutoa bidhaa inayoitwa ASPIRE ACCOUNT kwa lengo la kutoa morali ya kutumia huduma za kibenki kwa wanafunzi wa sekondari na vyuo.
Hafla hiyo fupi ilifanyika Januari 6,2012 kwenye hotel ya Golden Rose kwenye ukumbi wa Masaai hall, ambapo ilifuatiwa na tafrija fupi baadae.

Faida za wanafunzi kujiunga na bidhaa hizo ni kupata kadi ya mashine ( ATM) bure, hakuna makato ya mwezi, na kupata faida ya asilimia tano kila mwaka.

Pia bank hii imepunguza masharti kwa wanafunzi kufungua bidhaa hiyo ambapo hutoa vitambulisho vya shule pamoja na barua ya utambulisho kutoka  kwa wakuu wa shule na inafunguliwa kwa zero balance ama kiwango cha kuanzia elfu kumi kwa mwanafunzi atakayemudu kutoa kiwango hicho.


Picha ya pamoja baina ya washindi wa bidhaa hiyo awamu ya kwanza pamoja na washindi wa awamu ya pili, ambapo awamu ya kwanza washindi hao walipewa zawadi za flash, Ipod, pamoja na t shirt kutoka katika benki hiyo.
 Mshindi wa kwanza Jackline Swai (kulia) akikabidhiwa zawadi ya Lap top na Msadizi wa Meneja wa Azania Bank Tawi la Mbauda Hashim Ally Simchimbey.
 Mshindi wa Pili Ramadhani Mkorehe (kulia) akikabidhiwa zawadi ya Lap top na Msaidizi wa Meneja wa Azania Bank Tawi la Mbauda Hashim Ally Simchimbey
 Ulifika wakati wa msosi na hapa washindi wakiongozwa na Kirigiti Chacha Wamburawakijipakulia msosi.
 Ilikuwa ni makulaji tu

No comments:

Post a Comment