July 15, 2011

Mbowe aikaribisha Januari Makamba Chadema

Mwenyekiti wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini hii leo amemuoamba Mwenyekiti wa Kamati ay Bunge ya Nishati na Madini Januari Makamba na kamati yake yote kuhamia CHADEMA ili mikakati yake iwe na nguvu katika kulinusuru taifa. 

Ipo haja kwa Rais kutenganisha Wizara ya Nishati na Madini na kuzifanya kuwa mbili ili kuleta ufanisi. hata hivyo mchangiaji wa pili wa hutuba hiyo ya Bajeji, Mbunge wa Mbinga Gaudence Kayombo alishangaa kauli hiyo ya Mbowe na kudai kuwa Serikali ya awamu ya nne ilipunguza Wizara ili kupunguza matumizi ya serikali sasa inakuaje yeye atake tena kuongeza. Mbowe alisema amesema hivyo kwa nia nzuri ya kuisaidia serikali.

Aidha Waziri  wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisimama na kumweleza Mbowe kuwa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge inayoongozwa na Makamba si Kamati ya CCM bali ni ya Bunge.

Bunge leo limeanza kujadili Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ambapo Mbowe alikuw mchangiaji wa kwanza katika Hotuba hiyo.

No comments:

Post a Comment