
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge Dar es Salaam akifagia zualia kabla ya Rais Jakaya Kikwete kuwasili shuleni hapo katika kituo namba moja cha kujiandikisha wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Rais Jakaya Kikwete akijiandikisha kwaajili ya uchaguzi wa serikali za Mtaa unaotaraji kufanyika baade mwezi huu katika Kituo namba moja, mtaa wa Kivukoni, kilichopo shule ya msingi Bunge Dar es Salaam Oktoba 5 2009,mchana. Kikwete alikuwa ni mwananchi wa 12 kujiandikisha tangu kuanza kwa zoezi hilo kituoni hapo jana. Kulia ni Mwalimu Issa Kipengele anaye mwandikisha.

Akiondoka baada ya kujiandisha. JK aliwahimiza wananchi kutumia haki yako ya kujiandikisha ili wapige kura kuwachagua viongozi wa serikali zao za Mtaa "Hawa ndio viongozi wenu wa kutatua shida na kero mbalimbali kwa ngazi ya mitaa yenu...maji taka mtaani, ugomvi usiku na mchana..." alisema Kikwete.
SIKUJUA BADO TUKO "ENZI ZA MWALIMU" ZA KUWATOA WATOTO DARASANI WAFANYE USAFI WA "ZIMA MOTO" ILI KUMRIDHISHA MUHESHIMIWA. MI NILIDHANI MAMBO HAYA YALIISHA ENZI HIZOOOOOO!!
ReplyDeleteJamani huyu si amezimia juzi kule Mwanza? Bado anatembea tembea tu?!?
ReplyDeleteKwani hilo daftari si angepelekewa ofisini kwake akasainia huko tu?
Muoneeni HURUMA mwenzenu jamani!