August 13, 2008

MSAADA KIBANDANI

WADAU WATUKUFU!

TAKRIBANA SIKU TATU ZIMEPITA NA http://www.michuzi-blog.com/ HAIKO HEWANI KUTOKANA NA CHANGAMOTO ZA KIUFUNDI ZA HOST WETU BLOGGER-GOOGLE AMBAYE ANA MATATIZO YA KUUNGANISHA FTP SERVER YAKE NA GLOBU KIBAO IKIWEMO HII YA JAMII. HIVYO WAKATI TUKISUBURI MAMBO YAKAE SAWA MUDA SI MREFU UJAO, LIBENEKE LINAENDELEA KULE KWA ZAMANI AMBAKO NI http://www.issamichuzi.blogspot.com/.

NAOMBA RADHI KWA CHANGAMOTO HII AMBAYO IKO NJE YA UWEZO WETU NA WAHANDISI WA GOOGLE WAMENIHAKIKISHIA KWAMBA MAMBO YATAKUWA MSWANO PUNDE TU NA WAMEOMBA UVUMILIVU WAKATI HUU AMBAPO WANATAFUTA SULUHISHO LA KUDUMU ILI KWIKIWI ISITOKEE TENA HUKO MBELENI.

SAMAHANI KWA USUMBUFU WOWOTE ULIOPATIKANA

MUHIDIN ISSA MICHUZI

1 comment:

  1. blog imerudi hewani tayari. angalia www.michuzi-blog.com

    ReplyDelete