August 08, 2008

Jimmy Elias Afariki Dunia


Mwandishi wa siku nyingi Jimmy Elias afariki
Na Mwandishi Wetu
MWANDISHI wa habari wa siku nyingi, Bw. Jimmy Elias (41) amefariki dunia juzi asubuhi katika Hospitali ya Amana, Dar es Salaam, baada kuugua kwa takribani mwezi mmoja.
Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, mmoja wa ndugu wa marehemu, Bw. Richard Mwaikenda, alisema Jimmy (pichani) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya matumbo na alikuwa akiendelea na matibabu nyumbani lakini alipozidiwa alipelekwa Hospitali ya Amana kwa matibabu zaidi.
Mwili wa marehemu unatarajia kuagwa leo mchana saa sita (kesho) nyumbani kwake Kiwalani Bombom na baadaye kusafirishwa kuelekea katika kijiji alipozaliwa Ngana, wilayani Rungwe mkoani Mbeya tayari kwa mazishi yatakayofanyika kesho (Jumapili).
Bw. Mwaikenda alisema hadi mauti yanamkuta alikuwa Meneja Mauzo wa gazeti la Ngurumo za Simba na jarida la StarSport tangu yalipoanzishwa.Alisema katika kipindi cha uhai wake aliwahi kuandikia magazeti ya Dar Leo (zamani Majira Jioni) na Mfanyakazi.
Aliongeza kuwa licha ya kuwa na taaluma ya uandishi wa habari, pia Jimmy alikuwa ni fundi umeme wa majumbani na alihitiumu mafunzo hayo katika katika Shule ya Ufundi ya Vituka, Temeke, Dar es Salaam.
Marehemu ameacha mjane Bi. Mary Katendele na watoto watatu ambao ni Boniface, Jackson na Staford.
Katika uhai wake alikuwa mpezi mkubwa wa mpira wa miguu ambapo alikuwa ni mwanachama hai wa Klabu ya Simba.mwisho

1 comment:

  1. Ooooooh masikini Jimmy, Nakukumbuka sana ndio mlionipokea Business Times enzi hizo, Pole Kaka Richard Mwaikenda na familia ya wanahabari kwa ujumla.
    Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.
    Pius

    ReplyDelete