July 02, 2008

Bingwa wa Celtel

Meneja wa Huduma za Jamii wa Celtel Tanzania, Tunu Kavishe (kushoto) akikabidhi kombe kwa kocha wa timu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Lauren Ndumbaro, Dar es Saalam hivi karibuni kutokana na timu hiyo kufika robo fainali ya mashindano ya kitaaluma ya Celtel Africa Challenge ya vyuo vikuu yaliyofikia tamati Kampala, Uganda. Chuo Kikuu cha Engbert cha Uganda kiliibuka mshindi wa mashindano hayo yaliyoshirikisha pia vyuo kutoka nchi za Kenya, Malawi, na Zambia, na kupata zawadi anuwai zenye thamani ya dola 50,000.
Meneja wa Huduma za Jamii wa Celtel Tanzania, Tunu Kavishe (kushoto) akikabidhi kombe kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki, Profesa Keto Mshigeni, Dar es Saalam hivi karibuni kutokana na timu ya chuo hicho kufika nusu fainali ya mashindano ya kitaaluma ya Celtel Africa Challenge ya vyuo vikuu yaliyofikia tamati Kampala, Uganda. Mashindano hayo pia yalishirikisha vyuo kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, na Zambia.

2 comments:

  1. AnonymousJuly 03, 2008

    Tanzania tujifunze kutokana na makosa next time tushinde sisi sasa maana Kenya na Uganda wameshashinda tuanze mazoezi sasa current affairs etc through websites

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2008

    Deat Tunu, Jamani mbona umenenepa hivyo! Please usiongezeke dear

    ReplyDelete