Nafasi Ya Matangazo

June 13, 2024





Shirika lisilo la kiserikali linalojihususha na utoaji wa misaada kwa Jamii Good Neibhours Tanzania imeandaa Mafunzo maalumu kwa walimu wa masomo ya Sayansi,Hesabu na Kiingereza kwa shule za Sekondari Kimbiji na Pembamnanzi ,Mafunzo ni ya siku tatu kuanzia tarehe 11 June-13 June  yanayofanyika katika fukwe ya bahari ukumbi wa Barakuda

Aidha lengo la kuandaa Mafunzo hayo ni kuwajengea walimu hao uwezo wa Umahiri katika Mtaala Mpya ulioboreshwa  katika  masomo  na ufundishaji.

 Mafunzo hayo ambayo yalifunguliwa na Bi,Twidike Ntwima Afisa Elimu kata ya Kimbiji Amesema 

"Kipekee nawapongeza na kuwashukuru  sana shirika la Good Neibhours Tanzania Kwa kuandaa Mafunzo haya ya kuwajengea uwezo walimu wa masomo ya Sayansi,Hesabu na  Kiingereza na ameomba  wawe na muendelezo wa kuandaa semina  mara kwa mara kwani kupitia Mafunzo haya wanafunzi watanufaika kwa kuongeza ufaulu kwa kupitia Ujuzi ,maarifa na mbinu walizozipata walimu katika mafunzo.

Pia nimewataka  walimu waliopata  Mafunzo haya yakawe chachu kwa walimu wengine na pia kuwafundisha wanafunzi wa juhudi zote na kutumia mtaala wa Umahiri yaani (Competence -Based Curriculum),Alisema Bi Twidike Ntwima Afisa Elimu kata ya Kimbiji.

"Kipekee kama shirika Letu lilivyo Tunaendelea kutoa misaada mbalimbali katika Jamii yetu leo tumeandaa Mafunzo haya maalum  kwa walimu wa 20 wa Sekondari Kimbiji na Pembamnanzi Lengo kuu ni kuwajengea uwezo kuweza kutumia mbinu mbalimbali 
za mtaala wa Umahiri tunafahamu Mtaala  imedhamiria wanafunzi wafundishwe mbinu shirikishi.

Pia kuwajengea uwezo wa namna ya kutumia mihutasari kwani ndiyo msingi wa masomo katika ufundishaji,, Alisema Bi.Anameleni Christian mkufunzi mwandamizi wa shirika la Good Neibhours.
Posted by MROKI On Thursday, June 13, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo