Nafasi Ya Matangazo

May 01, 2024





Na Eleuteri Mangi, Arusha 
Wanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha wamefanya matendo ya huruma kwa kutoa fedha na vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh. 11,557,000/= ambavyo vimekabidhiwa kwa vituo vinne vyenye uhitaji maalum.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Michezo ya Mei Mosi Taifa Bi. Roselyne Massam Aprili 30, 2024 jijini Arusha wakati wanamichezo hao wanakabidhi msaada huo kwa vituo vya Kindness Orphanage, The Joy of God Orphanage, Umwaisha Children Home pamoja na kituo cha Wazee cha Meru Elderly Initiative ili wapate mahitaji ya msingi ya kila siku katika maisha yao.

Akikabidhi mahitaji hayo Mwenyekiti huyo amesema ni utaratibu wa kila mwaka wanamichezo hao kutoa sehemu ya fedha zao kusaidia wahitaji kwa kufanya matendo ya huruma mkoa ambao maadhimisho ya Mei Mosi Taifa mwaka husika yanafanyika.

“Tendo hili nla huruma kwa wahitaji ambao wapo kwenye mkoa mwenyeji ambao michezo inafanyika kuelekea maadhimisho ya Mei Mos Taifa mwaka huo na Arusha tumejipanga kuwapa mahitaji vituo vinne, mtambue wanamichezo tunawapenda. Tumeona ni vizuri tushiriki kwa kuchanga michango yao binafsi kwa mahitaji ya moja kwa moja ambayo tunayanunua na mahitaji mengine ambayo yanahitajika kwenye vituo vyetu” amesema Bi. Roselyne.

Vitu vilivyokabidhiwa ni vyakula kama mchele, unga wa ngano na mahindi, mafuta ya kupikia, sabuni za kufulia na kuogea, mahitaji ya shule kwa wanafunzi yakiwemo madaftari, kalamu, penseli, juice, taulo za kike, pampasi vitu ambavyo vimegawiwa sawa kulingana na mahitaji pamoja na umeme wenye thamani ya Sh. 150,000/= kwa kila kituo

Aidha, vituo hivyo vimekabidhiwa fedha tasllimu zitakazowasaidia kuendesha vituo hivyo kulingana na mahitaji yao. Kindness Orphanage ambacho kinalea mabinti kimepewa pesa taslimu kiasi cha Sh. 800,000/=, The Joy of God Orphanage kimepewa pesa taslimu kiasi cha Sh. 600,000/=, Umwaisha Children Home kimepewa pesa taslimu kiasi cha Sh. 500,000/= na kituo cha Wazee cha Meru Elderly Initiative kimepewa pesa taslimu kiasi cha Sh. 500,000/=.

Kwa upande wake Sr. Janeth Ngopa mlezi wa kituo cha kulea Watoto cha The Joy of God Orphanage cha jijini Arusha amewashukuru wanamichezo hao kwa moyo wao wa majitoleo na kukichagua kituo hicho kuwa miongoni mwa vituo vilivyopokea msaada na wameipokea kwa furaha na moyo wa shukrani.

 Sr. Janeth ameongeza kuwa ujio wa wanamichezo hao jijini Arusha umekuwa furaha, baraka na mafanikio kwao na watoto wanaolelewa katika vituo hivyo na ameishukuru Serikali kuuchagua mkoa wa Arusha kwa mwenyeji wa Siku Kuu ya Wafanyakazi kitaifa mwaka huu.
Posted by MROKI On Wednesday, May 01, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo