Nafasi Ya Matangazo

October 13, 2021

 

Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete akiwa na viongozi wengine mbalimbali wa Mkoa wa Pwani wakiwa katika ziara Makamu wa Rais Dr.Philip Mpango tumetembelea  mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere kujionea Maendeleo ya Mradi. 

Makamu wa Rais Dk Philip Mpango (wapili Kulia) akizungumza jambo wakati wa ziara hiyo. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Oktoba 12,2021 ametembelea mradi  wa ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere katika mto Rufiji, mradi unaogharimu shilingi Trioni 6.58.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo, Makamu wa Rais ameipongeza wizara ya Nishati, Wakandarasi pamoja na wafanyakazi wote wanaoshiriki katika ujenzi wa mradi huo. Amesema mradi huo ni mkombozi katika sekta ya nishati nchini hivyo amewataka viongozi na wote wanaohusika katika mradi huo kuwa wazalendo na kutanguliza maslahi ya taifa wakati wote.

Amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha mradi huo unakamilika kama ilivyopangwa na hivyo ameagiza wakandarasi kuwa makini na kutatuta hitilafu yeyote itakayojitokeza mapema ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza baadae katika mradi huo.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameagiza viongozi wa mikoa na wilaya zote inakopita mito inayotiririsha maji katika mto Rufiji kutunza mito hiyo na kutoa elimu kwa wananchi ili kulinda mazingira kwa manufaa ya mradi huo.

Posted by MROKI On Wednesday, October 13, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo