Nafasi Ya Matangazo

October 24, 2021

 


Mwandishi wetu,
Arusha. Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imepata tuzo ya taasisi ya afya inayoongoza kwa matumizi ya tehama kwenye utoaji wa huduma na shughuli za kila siku.

Tuzo hiyo imetolewa wakati wa mkutano wa tano wa tehama uliofanyika jijini Arusha ukiandaliea na Tume ya Tehama.

JKCI imepata tuzo hiyo baada ya Tume ya Tehama kufanya ukaguzi na kubaini kuwa asilimia 90 ya huduma za taasisi hiyo zinatolewa kwa mifumo ya tehama.

Mkuu wa Idara  ya Tehama JKCI Raymond Machari amesema taasisi hiyo imejiwekeza katika kutumia tehama katika kila huduma.

“Pale JKCI kuanzia mgonjwa anapofikishwa ataandikishwa kwa mfumo wa tehama, njia hiyo hiyo itatumika anapokwenda kwa daktari hadi kufikia hatua ya kuchukua dawa. 

“Ukiacha hilo pale tuna mfumo wa kufuatilia malalamiko, changamoto yani kuna namba maalum endapo mgonjwa amefika labda ameombwa rushwa au hajapatiwa huduma,” amesema Machari.

Kando na hilo taasisi hiyo pia ina mfumo unaowafuatilia na kuwakumbusha wagonjwa wake kuhudhuria kliniki.

“Kuna utafiti ulifanyika ukaonyeshwa watu wengi wanapoteza maisha kwa kutokamilisha matibabu na matumizi ya dawa.

“JKCI tukaona tuwe na mfumo ambao utatuwezesha kuwakumbusha wale wagonjwa wetu wanaokuja kliniki. Yani kama kliniki ni kesho leo mgonjwa anapata ujumbe kwenye simu yake,”.
Posted by MROKI On Sunday, October 24, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo