Nafasi Ya Matangazo

January 17, 2018


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari, mradi unatekelezwa katika eneo la Kingo ya Bahari iliyopo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) yenye urefu takribani mita 500. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira a Muungano January Makamba. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano January Makamba akizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Rais ya kukagua maendeleo ya mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari katika eneo la Kingo ya Bahari iliyopo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) yenye urefu takribani mita 500 leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akielezea jambo wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ya kukagua maendeleo ya mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari, mradi ambao unatekelezwa katika eneo la Kingo ya Bahari iliyopo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) yenye urefu takribani mita 500. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari kutoka kwa mmoja wa wakandarasi wa mradi huo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi huo leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo wa Kuimarisha Kingo za Bahari unatekelezwa katika kingo za Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA) Kigamboni yenye urefu wa mita 500, Sea View yenye urefu wa mita 900, Pangani Tanga na Zanzibar Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipita juu ya Kingo ya Bahari iliyojengwa kupitia mradi wa uimarishaji wa Kingo za Bahari alipotembelea Fukwe ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo. Fukwe hiyo imefanyiwa maboresho ambapo kingo yake imejengewa njia ya wapita kwa miguu na sehemu za kupumzikia. Sehemu ya Kingo iliyojengwa katika fukwe ya bahari ya hindi eneo la Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Siasa wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Kigamboni alipokutana nao wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari, mradi unaotekelezwa katika eneo la Kingo ya Bahari iliyopo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) yenye urefu takribani mita 500. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Kate Mfutakamba. (Picha na Frank Shija – MAELEZO)
Posted by MROKI On Wednesday, January 17, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo