Nafasi Ya Matangazo

November 16, 2017

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kasongati Alfan Kabika akitoa kiliovhake kwa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Pamoja na ujumbe wake juu ya kuboreshewa miundombinu katika Soko laujirani Mwema kati ya wananchi wa Burundi name Tanzania.
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
WANANCHI wa vijijiiji vya Kikulazo na Kasongati Wilayani Kakonko Wameiomba Serikali ya wilaya hiyo  Kuchukua baadhi ya Miundombinu Katika Soko hilo ambayo ni changamoto ikiwa ni pamaoja na Upungufua wa vyoo, ubovu wa Barabara na vibanda vitakavyo tumika kuwekea bidhaa za Wananchi hao.

Akizungumza juzi katika Soko la ujirani mwema linalowaunganisha Raia Wa Burundi na Watanzania kufanya biashara , mwenyekiti wa Kijiji cha Kasongati Alfan Kabika alimuomba Mkurugenzi kuwasaidia kurejesha baadhi ya fedha zinazo kusanywa kupitia kodi ya Wananchi hao kwani soko hilo ni moja kati ya vyanzo vikubwa vinavyo ongoza katika makusanyo na pato la Halmashauri.

Alisema Soko hilo limesaidia sana kupunguza masuala ya uvamizi kwani Warundi wengi wanatumia soko hilo kupata mazao waliyokuwa wakiingia katika kijiji hicho na kuwaibia mazao na fedha zao kwa kipindi cha nyuma lakini tangu kuanzishwa kwa soko hilo uhalifu umepungua.

Hata hivyo kibika alisema kufuatia muingiliano wa Warundi katika biashara walianzisha ulinzi wa nyumba kumi, na kuwa na utaratibu wa kutambua wageni wa Kijiji wanaoingia na kutoa taarifa kwa Viongozi waweze tambua na Wananchi wameitikia mpaka sasa hakuna uharifu katika Kijiji hicho.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala, alisema alisema Masoko mengi ya mpakani yana kuwa watu wengi lakini masoko hayo yana vyoo vichache zaidi ya Watu 5000 wanaingia katika soko hilo lakini soko lina vyoo viwili tuu  jambo ambalo ni hatarishi kwa magonjwa ya tumbo kutokana na hali iliyopo.

Aidha Kanali Ndagala alitoa agizo kujengwa kwa vyoo ndani ya wiki moja endapo watashindwa kujenga vyoo katika soko hilo atalifunga soko hilo na hawawezi kuona wananchi wanaangamia kwa magonjwa yatokanayo na ukosefu wa Vyoo.

Alisema Masoko hayo yamekuwa yakiwasaidia Wabanchi kuongeza kipato na kupitia masoko hayo yamesaidia sana kupunguza uhalifu uliokuwa ukifanywa na baadhi ya raia kutoka nje, imesaidia kujenga uhusiano mzuri baina ya wananchi wa Tanzania na Warundi kutokana na ujirani mwema huo na kuagiza huduma ziboreshwe katika maeneo hayo.

" niwaombe wananchi kupitia uhusiano huu muhakikishe mnafuata utaratibu, viongozi mtumie fursa hii ya masoko ya ujirani mwema kuwaelekeza Wananchi kufuata utaratibu wa kuchukua vibari kabla ya kuingia Nchi jirani na Warundi wanapoingia Nchini pia wafuate utaratibu huo hii itatusaidia kupunguza uhalifu pia katika masoko hayo", alisema Ndagala.
Posted by MROKI On Thursday, November 16, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo