Nafasi Ya Matangazo

October 13, 2017

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga amewahimiza wakazi wa Wilaya ya  Kakonko kuzalisha zao la pamba  kwa ubora na kuimarisha ushirika ili kuongeza uchumi wa kila mwananchi.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Kanyonza baada ya kufanya ziara   alieleza kuwa, Serikali imetoa bei elekezi ya kununua mbolea ambapo mbolea ya kupandia DAP itauzwa kwa ruzuku ya serikali kwa  shilingi 55741  na mbolea ya kukuzia UREA itauzwa kwa shilingi 43169.

Alisema  awali mbolea hizi zilikuwa zikiuzwa kati ya sh.55,000 hadi 80,000. Mhe.Maganga amefafanua kuwa kwa sasa mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kiwango cha umaskini ambao ni asilimia 48.4.

Aidha Mkuu wa mkoa aliwataka wananchi kutii sheria bila shuruti kwa kuepuka kilimo cha bangi kwani heka 8 za bangi zilikamatwa wilayani Kakonko mwaka Jana 2016 na wote waliokuwa wakilima bhangi walikuwa wakichanganya na mazao mengine.

" niwaagize wananchi yeyote atakae kamatwa akilima bhangi katika shamba lake  atachukuliwa hatua za kisheria, mazao ya kulima ni mengi na yanaweza kuinua uchumi wenu jiepusheni na mazao yasio faa mnaweza kuhalibu vizazi vyenu vijavyo jitahidini kufuata sheria za nchi mfanye kilimo chenye yija", alisema mkuu huyo.

Vilevile amekemea vitendo vya wananchi kuchukua sheria mkononi kwa kuua watu wengine hasa wazee kwa tuhuma za ushirikina. Ametoa wito kwa watu wa Burundi wanaoishi kama wakimbizi nchini Tanzania kuishi kwa amani na watanzania na kuepuka kufanya mauaji na vitendo vya uporaji. Ameeleza kuwa tabia hiyo ikiendelea ataomba kibali  kwa Rais kuwarudisha walipotoka wakimbizi nao.

Hata hivyo  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala alisema atahakikisha anawahimiza maafisa ugani wahakikishe wanawatembelea wakulima na kuanzisha mashamba darasa iliwaweze kuzalisha pamba za kutosha iliwananchi waweze kuongeza uchumi wao.

Alisema kwa mwaka uliopita Wananchi wa Wilaya hiyo baadhi walilima pamba na wengi wao kilimo hicho kiliinua uchumi wao kwa asilimia 75% na kwa mwaka huu watahakikisha wanatoa pembejeo na elimu ya kutosha kwa Wananchi wanaweza kulima kitaalamu.

Mhe. Maganga amefanya ziara ya kikazi kwa kutembelea wakulima wa pamba  katika kata ya kanyonza, kiziguzigu na anaendelea na ziara yake siku ya jumatano .
Posted by MROKI On Friday, October 13, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo