Nafasi Ya Matangazo

March 12, 2017

Na Pamela Mollel,Arusha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bi.Jennista Mhagama amewataka vijana kujiepusha na madawa ya kulevya ili utekelezaji wa dhana ya Tanzania ya viwanda ilete ajira kwa vijana wenye nguvu

Aliyasema hayo jijini Arusha wakati akifunga mkutano mkuu wa9 wa wadau
 wa mfuko wa hifadhi ya watumishi wa serikali za mita,  LAPF uliohudhuriwa na wadau wa mfuko huo

Alisema kuwa kwa sasa serikali imedhamiria kuwainua idadi kubwa ya vijana waliona ujuzu mdogo kwa kuwajenge uwezo kupitia mafunzo mbalimbali katika vyuo vilivyopo nchini

''Udhibiti mkubwa wa madawa ya kulevya unahitajika kwa vijana wetu ili kutengeneza taifa lenye nguvu ya kufanya kazi ''alisema

Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya watanzania hawana ujuzi wa kutosha hivyo basi serikali ya awamu ya 5 imejipanga ipasavyo kuhakikisha vijana wanapata ajira kupitia viwanda

Hata hivyo aliipongeza mfuko wa LAPF kwa kazi nzuri wanayofanya huku akiitaka mifuko yote ya kijamii hapa nchini ihakikishe kuwa ifikapo 2025 inakuwa na wanachama wengi zaidi
Posted by MROKI On Sunday, March 12, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo