Nafasi Ya Matangazo

March 29, 2017


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAIMU Katibu Mkuu wa  Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati Shirika la  Umeme Tanzania (TANESCO), likifanya jitihada za kufanya uchunguzi  katika mfumo mzima wa Gridi ya Taifa na kurekebisha hitilafu iliyopelekea kukosekana kwa umeme katika mikoa yote iliyounganishwa na Gridi  ya Taifa leo hii Machi 29, 2017.
Kwa mujibu wa taarifa ya TANESCO kutoka kitengo cha Uhusiano Makao Makuu, imemnukuu Profesa Mdoe, (pichani juu katikati) akiyasema hayo mbele ya Waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kutembelea Mitambo ya umeme wa Gesi ya Kinyerezi I ili kufuatilia tatizo la kukatika kwa umeme katika mikoa yote iliyounganishwa na Gridi ya  Taifa saa 1:00 asubuhi leo Machi 29, 2017.
Alisema mara baada ya wataalam kutoka TANESCO kugundua hitilafu,  walianza kushughulikia tatizo hilo na kufanikisha kurejesha umeme katika mikoa ya Iringa ambayo ilipata umeme saa 1:27, Dar es Salaam saa 1: 43 pamoja na Zanzibar ambayo ilipata umeme saa 2: 42 na kuongeza kuwa ilipofika saa 6 mchana mikoa yote iliyounganishwa na Gridi ya Taifa ilipata umeme kama kawaida.
Alieleza kuwa uwashaji wa mitambo unaendelea na uchunguzi wa kubaini chanzo cha hitilafu bado unaendelea.
Wakati huo huo Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji (anayeshughulikia usafirishaji umeme), Mhandisi Kahitwa Bishaija alisema mpaka sasa tatizo limeshadhibitiwa na kwamba wanaendelea na uchunguzi chanzo cha tatizo hilo ili kudhibiti lisitokee tena.


Profesa Mdoe, akiagana na viongozi wa TANESCO baada ya ziara yake ya ghafla kwenye mitambo ya umeme wa Gesi, Kinyerezi jijini Dar es Salaam. (PICHA NA TANESCO)
 Eneo la mitambo ya umeme wa Gesi Kinyerezi jijini Dar es Salaam
Posted by MROKI On Wednesday, March 29, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo