Nafasi Ya Matangazo

February 02, 2017

Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde akijibu maswali yaliyoulizwa na kuelekezwa katika Wizara yake Bungeni Mjini Dodoma leo.
                                                                        ************
Naibu Waziri Anthony Mavunde amewataka vijana wote wenye nia ya kufanya shughuli za kilimo,ufugaji na ujasiriamali kubuni miradi yenye tija na kutumia fursa iliyopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kukopa fedha zitakazowasaidia katika kuendesha shughuli zao mbalimbali,ambapo mpaka sasa takribani sh 1.7 bn zineshatolewa kwa vikundi mbalimbali vya Vijana nchini.

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo wakati akijibi swali la Mh Hassan Elias Masala-Mbunge wa Nachingwea aliyetaka kujua mipango ya serikali katika kuwakwamua Vijana wa Wilaya ya Nachingwea katika wimbi  la ukosefu wa Ajira.

Naibu Waziri Mavunde alimuomba Mh Masala kuwasaidia vijana kukaa katika vikundi ili wasajiliwe na baadaye waweze kukopeshwa.
Posted by MROKI On Thursday, February 02, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo