Nafasi Ya Matangazo

September 21, 2016Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi
 WATU 13 wamepoteza maisha na wengine 11 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyoyahusisha magarui mawili ya abiria kugongana katika eneo la Mwamaya Wilayani Kwimba mkoani Mwanza leo asubuhi.

Akizungumza na Habarileo online, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo tukio na kusema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya Saa 12:15 asubuhi na ilihusisha gari dogo la abiria Toyota Hiace lenye namba za usajili T368 CWQ lililokuwa likotokea kijiji cha Shirima kwenda Mwanza mjini na kugonagana na Basi aina ya Scania lenye namba za usajili T874 CWE.

 Kamanda Msangi alisema kuwa ajali hiyo ilitokea wakati gari hilo dogo likiingia katika barabara kubwa na kugongana na basi hilo lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Mwanza na kusababisha vifo hivyo kwa abiria na majeruhi waliokuwa katika gari hilo dogo.

“Nipo njiani naenda eneo la tukio lakini taarifa za awali nilizopokea ni kuwa watu 13 wamefariki duniani na wengine 11 wamejeruhiwa na kati ya hao marehemu wawili ni watoto wadogo, na ajali imetokea katika makutano ya barabara kuu na hiyo ya kutokea kijiji cha Shirima ili pokuwa ikitokea gari ndogo.SOURCE: Habarileo Online.
Posted by MROKI On Wednesday, September 21, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo