Afisa Mwandamizi kutoka Kitengo cha Elimu katika Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani , ASP. Mossi Ndozero akitoa Elimu ya usalama barabarani kwa baadhi ya walimu wa shule za Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika katika Chuo cha Polisi Wanamaji jijini Mwanza yaliyoendeshwa na jeshi hilo chini ya udhamini wa kampuni ya TBL Group.
Baadhi ya walimu wakifanya mazoezi katika makundi.
SGT Bahati Nzunda akitoa somo kwa walimu wakati wa mafunzo hayo.
Walimu wakifuatilia mafunzo ya usalama barabarani.
Afisa Mwandamizi kutoka Kitengo cha Elimu katika Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani , ASP. Mossi Ndozero akitoa Elimu ya usalama barabarani kwa baadhi ya walimu wa shule za Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika katika Chuo cha Polisi Wanamaji jijini Mwanza yaliyoendeshwa na jeshi hilo chini ya udhamini wa kampuni ya TBL Group. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
*************
KAMPUNI ya TBL Group imetangaza kuwa itaendelea kutoa elimu ya Usalama katika maeneo yake ya kazi na kwa jamii ili kuhakikisha matukio ya ajali zisizo za lazima zinapungua hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Usalama kazini wa kiwanda cha TBL cha mjini Mwanza,Bw.Method Marco wakati akielezea mafunzo ya usalama ambayo yamefadhiliwa na kampuni kwa ajili ya walimu wa shule za msingi na sekondari na wakaguzi wa magari kutoka Jeshi la polisi nchini mkoani humo.
Bw.Method alisema linapokuja suala la usalama na afya haliwahusu wafanyakazi wa kampuni na familia zao tu bali kwa jamii nzima kwa kuwa wafanyakazi wa TBL Group ni sehemu ya jamii na wanaishi kwenye jamii.
“Sera za kampuni yetu zinahimiza kulipa kipaumbele mkubwa suala la Usalama na afya sio kwa wafanyakazi tu bali usalama wa jamii nzima na ndio maana kampuni imekuwa mstari wa mbele kufadhili na kushiriki katika kampeni mbalimbali za usalama na miradi ya Afya na Mazingira”.Alisema Marco.
Kuhusiana na ufadhili wa semina ya wakaguzi wa magari kutoka Jeshi la polisi na walimu wa shule za msingi na ekondari alisema kuwa kampuni imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na taasisi hizo kuhusiana na masuala ya usalama hususani kampeni za usalama barabarani lengo kubwa likiwa ni kupunguza matukio ya ajali nchini.
Moja ya lengo lengo letu tunalotekeleza ni kuhamasisha unywaji wa kistaarabu kwa jamii hivyo kama kampuni inayotengeneza vinywaji tunalo jukumu la kuelimisha masuala ya usalama kwa ujumla na tunaamini Jeshi la polisi kama msimamizi wa masuala ya usalama barabarani nchini linapaswa kuungwa mkono na kupewa ushirikiano mkubwa kuhakikisha linafanikisha kufikisha elimu ya usalama na usalama barabarani kwa wananchi wengi.
Kwa upande wa walimu na wanafunzi alisema kuwa kampuni itaendelea kushirikiana nao ikiwemo wadau wengine kuhakikisha wanapata elimu ya usalama barabarani “Ukifundisha walimu ni rahisi elimu hii kuwafikia wengi na wanafunzi wakipata elimu ya awali ya masuala ya usalama na usalama barabarani wanakua wakiwa na uelewa mpana wa kujikinga na kuchukua tahadhari.
Alisema suala la kuelimisha jamii kuhusiana na usalama barabarani ni jambo ambalo kampuni ya TBL Group itaendelea kulivalia njuga kwa nguvu zote kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na wadau wengine.
0 comments:
Post a Comment