Nafasi Ya Matangazo

June 19, 2016

 Wakulima wa Shahiri wakitembeza wageni mashambani
Wakulima wa zao la Shahiri kanda ya Kaskazini mwa Tanzania wanaoshirikiana na kampuni ya TBL Group wameadhimisha siku yao wilayani Karatu ambapo mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha wakiwemo wadau wao kutoka SABMiller,na makampuni mengine yanayouza  madawa na pembejeo za kilimo.

Wakulima waliweza kufanya maonyesho mbalimbali  ya kazi zao pia walielezea mafanikio walioweza kuyapata kutokana na kilimo cha zao la Shahiri
 Maofisa wa SABMiller na wafanyakazi wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo ambapo pia TBL Group ilitunukiwa tuzo kwa kendeleza kilimo cha zao la Shahiri nchini
 Mkuu wa  Uendelezaji Kilimo cha Shahiri wa SABMiller kanda ya Afrika Thinus  Van Schoor akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima wa Shahiri
 Naibu Waziri wa Kilimo,Chakula na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha (kulia) akimpongeza mkulima aliyejishindia zawadi ya kabati
 Naibu Waziri wa Kilimo,Chakula na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha (kushoto) akimpongeza mkulima wa Shayiri kutoka Kijiji cha Lendikinya wilaya ya Monduli,Masiaya Oloshuda aliyeshinda kwenye bahati nasibu ya kupata vifaa vya usalama shambani
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha akihutubia wananchi
Posted by MROKI On Sunday, June 19, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo