Nafasi Ya Matangazo

November 06, 2015

 Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli akiapa mbelea ya jaji mkuu wa Tanzania kiapo cha kuwa Rais wa Tanzania. Dk Magufuli amekula kiapo hii leo baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika nchini kote Oktoba 25, 2015 akigombea kupitia Chama cha Mapinduzi CCM. 
 
  Rais Dk.John Pombe Magufuli akila kiapo.
 Rais Dk. John Magufuli akisaini hati ya kiapo mbele ya Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande.
 Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande akisaini hati ya kiapo ya Rais Dk. John Magufuli.
 Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande akimkabidhi hati za kiapo Rais Dk. John Magufuli.
 Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli akipokea heshima ya kupigiwa wimbo wa taifa baada ya kuapishwa. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
  
 Rais Dk. John Magufuli akikagua kwaride lake la kwanza akiwa Rais wa Tanzania.
 Rais Dk. John Pombe Magufuli akitembea kikamavu baada ya kumaliza kukagua gwaride akiwa na Mkuu wa Majeshi, Generali Davis Mwamunyange.
 Rais Dk. John Magufuli akirejea jukwaa kuu.
 Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.
  Rais Dk. John Magufuli akipeana mkono na makamu wake Samia Suluhu Hassan.
  Rais Dk. John Magufuli, akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.
  Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na mkewe Mama Jannet Magufuli.

  Rais Dk. John Magufuli akipokea mkono wa pongezi kutoka kwa Rais Mstaafu wa awamu wa nne, Jakaya Mrisho Kikwete.
 
  Rais Dk. John Magufuli akimsikiliza Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa makini.
 
 Viongozi mbalimbali wakiwepo Wabunge wa Bumnge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Mabalozi, mawaziri Wakuu wastaafu na viongozi wengine mbalimbali wakifuatilia sherehe hizo katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhan Kailima pamoja na wajumbe wengine wa NEC wakifuatilia sherehe hizo.

Bilionea Aliko Dangote, Katibu Mkuu wa CCM, Comrade Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine wakifuatilia sherehe hizo. 
 
Viongozi mbalimbali wakiwepo Wabunge wa Bumnge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Mabalozi, mawaziri Wakuu wastaafu na viongozi wengine mbalimbali wakifuatilia sherehe hizo katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
 
Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dk John Pombe Magufuli, akipokea heshima. 
 Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi na Usalama, vikila kiapo cha Utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Ndege Vita zikitoa heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dk John Pombe Magufuli.
 Wakiangalia ndege vita hizo zikitoa heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.
 
 Viongozi na marais kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakisalimia

 Burudani toka vikundi mbalimbali zilitolewa.
 Rais Dk John magufuli na viongiozi wengine mbalimbali wakifuatilia matukio ya burudani.
 
 Burudani toka vikundi mbalimbali zilitolewa.
 Rais Dk. John Pombe Magufuli akisoma hotuba yake.
Rais Magufuli akiaga viongozi mbalimbali wakati akiondoka uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
 
  Rais Dk.John Magufuli akisalimia wageni wakati akiondoka. 
Posted by MROKI On Friday, November 06, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo