Nafasi Ya Matangazo

October 26, 2015


Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL), Abdulmaalik Mollel akizungumza na wazazi na wanafunzi wanaotarajia kuondoka Oktoba 28, 2015 kwenda kusoma masomo ya elimu ya juu wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam. 
Wazazi wakimsikiliza Abdulmaalik Mollel wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wazazi na wanafunzi  wanaokwenda nchini China kwa masomo ya elimu ya juu wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL), Abdulmaalik Mollel (hayupo pichani) wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL), Abdulmaalik Mollel akitoa nyaraka za taarifa za wanafunzi wanaokwenda nchini China wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi wakiuliza swali kwa masomo wanayokwenda kusoma katika vyuo vya nje wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL), Abdulmaalik Mollel akizungumza na mzazi wa mwanafunzi wa anyekwenda kusoma nchini China wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii. 

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. KAMPUNI ya Global Link Education imeendelea kupeleka wanafunzi kwenda kusoma vyuo vya nje vilivyo na uwezo kutoa elimu bora. Hayo ameyasema Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Link Education (GEL), Abdumaalik Mollel wakati akitoa mafunzo kwa wanafunzi 65 wanaokwenda nchini China kwa masomo ya elimu ya juu. 

Mollel amesema vyuo vya nje ambavyo vinashirikiana na GEL vina ubora wa elimu pamoja na kuwa na vitendea kazi vinavyoweza kufanya mwanafunzi afanye vizuri katika masomo yao. 

 Amesema wanafunzi 500, GEL imesha wadahili katika vyuo vya nje na wanafunzi hao wameona ubora wa vyuo hivyo na kuweza kuleta chachu ya maendeleo nchini kutokana na utaalam wataopata huko. Mollel amesema kuwa nafasi bado zipo katika vyuo vya China hivyo wazazi wanaweza kuwasiliana na GEL kufanya usajili katika vyuo hivyo. 

 “Nia ya GEL ni kuona wanafunzi wanafanya vizuri katika matokea na tunafatilia tabia zao hatua kwa hatua tukiwa na lengo ya kupata wasomi wenye ujuzi kwa maendeleo ya taifa”amesema Mollel. Aidha amesema kuwa wanafunzi wanaonyesha tabia mbaya wanawarudisha nchini katika kuweza kuokoa fedha za mzazi kuendelea kuhudumia mtoto ambaye mwishoni hatafanya vizuri.
Posted by MROKI On Monday, October 26, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo