Nafasi Ya Matangazo

August 29, 2015

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Njombe mjini katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa saba saba.Magufuli amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano ataendeleza juhudi zake za kujenga barabara kwa kiwango cha lami,amesema dhamira yake aliokuwa nayo ya Uwaziri wa Ujenzi katika kujenga barabara za lami katika maeneo yote hapa nchini.


Amesema tangu kupewa kuwa waziri wa ujenzi ameweza kujenga barabara  zaidi kilomita 7000 nchi nzima,ambapo ilipelekea kuongeza kuongeza pato la mfuko wa barabara kutoka bilioni 73,3 hadi kufikia bilini 866 kwa mwaka huu hivyo ameahidi akiwa rais atajenga zaidi barabara za lami.

Dkt MAGUFULI ambae anaendelea na mikutano ya kampeni za Urais mikoa ya nyanda za juu kusini , amelalamikia udanganyifu wa baadhi ya mitandao ya kijamii  na baadhi ya vyombo vya habari kuripoti  kuwa amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali ya mkoa wa mbeya wakati sio kweli.

Aidha pia Magufuli  amewaomba wananchi waweke imani kubwa kwake kwa  kumpa kura nyingi  zitakazomwezesha kuwa raisi wa awamu ya tano,na kIsha alipe fadhira hizo kwa kutatua kero zinazowakabili hasa wananchi wenye kipato cha chini.SOMA ZAIDI FK MATUKIO
Posted by MROKI On Saturday, August 29, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo