Nafasi Ya Matangazo

August 06, 2015

Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba akizungumza na Wandishi wa habari katika moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Peacok hotel jijini Dar leo kuhusiana na kung'atuka kwake rasmi Uenyekiti wa chama hicho na kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida,ambapo Mh Lipumba ameeleza kuwa yeye atabaki kuwa mwanachama hai na halali wa kawaida kwa sababu kadi yake ya uanachama ameshailipia mpaka mwaka 2020 

MWENYEKITI wa Taifa wa  Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho leo majira ya saa 5 asubuhi katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mbele ya waandishi habari,Pro.Lipumba amesema ametafakari sana katika kuendelea kuwa Mwenyekiti wa chama hicho lakini dhamira yake inamsuta.

Amesema kuwa mwaka 2014 hakutaka kugombea nafasi hiyo kutokana na mchakato wa katiba mpya akaamua kugombea kwa lengo ya kuwapa watanzania  katiba itakayoindoa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Lipumba amesema katika mchakato wa bunge maalumu wakaunda umoja wa katiba (UKAWA0 wenye lengo wa kusimamia katiba iliyopendekezwa lakini sasa waliopitisha ndio wanataka kuisimamia katiba hiyo ambayo haingii akilini.

Amesema alikuwa akishiriki vikao vya UKAWA lakini Aprili 1 mwaka huu alisema atang'atuka katika nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Wanannchi (CUF).

Amesema amepita katika misukosuko mingi katika kukijenga chama hadi kufikia kiasi hata kabambikiziwa  kesi ya kufanya maandamano bila kibali.

Lipumba amesema kazi yake atakuwa mwanachama wa kawaida, kufanya utafiti wa maendeleo endelevu  pamoja na kufanya ushauri wa masuala mbalimbali katika chama hicho. SOURCE:MICHUZI BLOG
Posted by MROKI On Thursday, August 06, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo