Nafasi Ya Matangazo

August 31, 2015

Na Woinde Shizza,Arusha
TIMU ya JKTMbweni kutoka Dar es salaam kwa  wanaume na wanawake zimefanikiwa kuchukuaubingwa wa wavu Tanzania msimu wa 2015 baada ya kufanya vyema katika mashindanoya klabu bingwa wavu  yalilomalizikajumamosi jijini hapa.

Mashindanohayo yaliyoendeshwa kwa mtindo wa ligi yalimalizika kwa timu kwa wanaume timuya Jkt Mbweni kummaliza mashindano hayo ikiwa na jumla ya pointi 15,ikifuatiwana timu ya Tanga ilijikusanyia jumla ya pointi 12,nafsi ya tatu iliwaendea timuya Pentagone ya Arusha kwa pointi 9 ,huku Dodoma wakipata jumla ya pointi 6,Karatu pointi 3 na timu ya Flowers ikikosa pointi na kushika mkia.

Maafande haowa JKT Mbweni pia kwa wanawake walimaliza mashindano hayo wakiwa na pointi6wakifuatiwa na Tanga kwa pointi 3  huku Dodomanao wakimaliza bila pointi.Michuanohiyo ya Klabu Bingwa wavu  Tanzaniailichezwa kwa siku tatu katika viwanja vya sheikh amri abeid pamoja na viwanjavya pentagone klabu huku ikiwa chini ya chama cha wavu mkoa wa Arusha (AVA) Pamojana chama cha wavu Tanzania (TAVA).

Akifunga mashindanohayo  mgeni rasmi ambaye alimuwakilishamkuu wa mkoa Arusha Mwanvita O. Okeng’o  ambaye ni afisa michezo mkoa aliwasihi wachezembalimbali kuongeza juhudi katika kuhakikisha wanahamasiha mchezo wa wavuunakuwa na wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu .Naye Makamomwenyekiti wa  chama cha wavu Tanzania(TAVA) Muharini Mchume alieleza kuwa pamoja na kuwa timu sita pekee ndizozimechuana vikali zimeweza kuonyesha ushindani wa kipekee kwani zilionekanakuchuana vilivyo.

“Mashindanoyamekwenda vizuri natunawashukuru chama cha wavu Arusha  (AVA)kwa maandalizi makubwa yaliyowezeshakufanyika kwa michuano hii vile vile shukrani kwa wazamini mbalimbaliwaliojitokeza kutuunga mkono’alisema  Aliongezakuwa mwenyekiti wa chama cha wavu Tanzania (TAVA) Augostino Hagapa hakuweza kufika kutokana na kuteuliwa kuwa ‘MatchCommissioner” katika mashindano ya wavu ya  All Africa Games yanayotarajiwa kuanza mapemamwezi septemba nchini Congo,akimuwakilisha Rais wa shirikisho la wavu Afrika. 

Aidha chamacha wwavu mkoa wa Arusha kimekabidhiwa mipira mitatu na chama cha wavu Tanzaniavile vile kilimkabidhi mgeni rasmi mpira mmoja kwa ajili ya mazoezi.

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo ya wavu 2014  timu yaMagereza kwa wanawake kutoka jijini Dar es salaam pamoja na timu ya BOT yajijini Mwanza kwa wanaumenazo pia hazikuweza.
Posted by MROKI On Monday, August 31, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo