Nafasi Ya Matangazo

July 11, 2015

WATANGAZA nia Dk John Pombe Magufuli,Dk Asha Rose Migiro na Balozi Amina Salum Ali wa Chama cha Mapinduzi CCM wamepeta kuingia hatua ya tatu bora na kuwatupa nje Bernard Membe na Januari Makamba. 

Watatu hao sasa wameingia katika kikaango cha mwisho cha Mkutano Mkuu ambapo watapigiwa kura na hatimaye kumpata moja ambae atapeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu. 

Duru za kisiasa zinampa nafasi kubwa ya ushindi Daktari Magufuli kufuatia utendaji wake wa kazi na hasa usimamizi wa miradi mbalimbali katika wizara yake ya Ujenzi.
Posted by MROKI On Saturday, July 11, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo