Nafasi Ya Matangazo

May 25, 2015

IMG_9411
Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Mbarouk Nassor Mbarouk(kushoto) akiwa katika swala iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika msikiti wa msikiti wa Alsahaba  ulioko eneo la Morombo jijini Arusha,ambapo aliwatembelea waumini hao na kutoa zawadi za tende.
**********
Waislamu kote nchini wametakiwa kujiandaa vyema na mwezi mtukufu wa Ramadhani unaotarajia kuanza hivi karibuni kwani kipindi hicho ni cha kufanya matendo mema na kuisaidia jamii hasa wahitaji.
 
Hayo yameelezwa  na Mwenyekiti wa taasisi ya  Islamic Foundation  Bader Marei  jana katika  swala ya ijumaa iliyofanyika katika msikiti wa Alsahaba  ulioko eneo la Morombo jijini hapa  na kuhudhiriwa na Balozi wa falme la kiarabu nchini .
 
Bader  huyo amesema kuwa kipindi cha Ramadhani ni kipindi cha kujitazama na kubadili mwenendo   na kuwa watu wanaofaa katika jamii.
 
Akizungumza kwa niaba ya Ugeni huo wa Ubalozi wa falme hizo za kiarabu amesema kuwa ziara hiyo inalenga kuangalia changamoto za kijamii na kuangalia namna ya kuzitatua ambapo wamezindua visima 34 vya maji katika wilaya ya Ngorongoro.
 
Mbali na shughuli hizo pia wamegawa msaada wa tende kwa waislamu wote waliohudhuria katika swala hiyo ikiwa ni moja kati ya maandalizi ya Mwenzi huo mtukukufu.
 
Baadhi ya waumini walioshiriki katika swala hiyo  Issa Tesha muuminI  na Saidi Hamis muumini  wameeleza kufurahishwa na ujio huo mkubwa ambao unashirikiana na jamii ya waislamu katika masuala mbali mbali ya kijamii na kidini.
 
“Tumefurahi kupata msaada wa tende kipindi cha Ramadhani upatikanaji wa tende huwa mgumu lakini sasa walau tuna tende tunashukuru sana “ Alisema Issa.Picha na Ferdinand Shayo wa jamiiblog.
Posted by MROKI On Monday, May 25, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo