Nafasi Ya Matangazo

December 11, 2014

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu (wapili kulia) na Balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto wakionesha ishara ya mshikamano baada ya Waziri Kabaka kuzindua huduma mbili za mikopo ya Elimu na mkopo wa kuanzia maisha kwa wanachama wa mfuko huo Dar es Salaam leo.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu (kulia) wakizindua huduma mbili za mikopo ya Elimu na mkopo wa kuanzia maisha kwa wanachama wa mfuko huo Dar es Salaam leo.
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi ambaye ndie alikuwa muongoza tukio hilo akizungumza.
 Balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hizo za mikopo ya elimu na kuanzia maisha kwa wanachama wa PSPF ukliofabnyika leo Da es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akizungumza.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu akizungumza kuhusiana n huduma hiyo mpya.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza wakati akizindua huduma hizo mbili kwa wanachama wa mfuko wa PSPF hii leo jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi wa TPB na PSFP wakiwa katika uzinduzi huo.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu (kushoto) wakizindua huduma mbili za mikopo ya Elimu na mkopo wa kuanzia maisha kwa wanachama wa mfuko huo Dar es Salaam jana.
  Wafanyakazi wa  PSFP wakiwa katika uzinduzi huo.


BAADA ya kuzindua huduma ya mikopo kwa wastaafu na kuleta mafanikio makubwa, Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania wamezindua huduma mpya kwa wateja wake, huduma hizo ni Mkopo wa kuazia Maisha na Mkopo wa elimu.

Kwa upande wa mkopo wa elimu mwanachama anaweza kukopa kwa ajili ya kujiendeleza kielimu katika ngazi yoyote ile ya elimu, mfano stashahada, shahada, shahada ya uzamili na hata mafunzo ya ufundi. Katika huduma hii PSPF imetenga jumla ya shilingi bilioni 4.

Kwa upande wa mkopo wa kuanzia maisha, mwanachama aliyepata ajira kwa mara ya kwanza huwa ana mahitaji muhimu, kwa kutambua hilo PSPF imeanzisha mpango huu ambapo mwanachama anaweza kukopa mishahara yake ya miezi miwili ili aweze kujipanga na maisha mapya ya ajira. Katika huduma hii PSPF imetenga jumla ya shilingi bilioni 2.

Lengo kubwa la PSPF kuanzisha mikopo hii ni kuhakikisha kila mtanzania anatimiza ndoto yake ikiwa ni katika masomo kwa kupitia mkopo wa elimu au ndoto yake nyingine kwa kupitia mkopo wa kuanzia maisha, hivyo natoa wito kwa watanzania  wenzetu kujiunga na PSPF ili waweze kufaidika na fursa hizi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri wa Kazi na Ajira Mheshimiwa Gaudentia kabaka alisema amefurahishwa na PSPF jinsi ilivyoshirikiana na Benki ya Posta Tanzania katika Kubuni, Kupanga, kuandaa na hatimaye kuteleza utratibu huu, alisema hili ni jambo sahihi na mwafaka kwani kwa mujibu wa taratibu za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii duniani kote, kazi za Mifuko hii sio kutoa mikopo bali ni kuwawezesha wanachama wake kupata mafao yao stahili pale wanastaafu. 

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba Moshingi alisema mwanachama wa PSPF anayetaka kukopa anatakiwa kwenda kwenye tawi lolote la Benki ya Posta lililopo karibu yake. Huduma za utoaji wa mikopo hii ni za haraka sana na bora.
Posted by MROKI On Thursday, December 11, 2014 1 comment

1 comment:

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo