Nafasi Ya Matangazo

November 21, 2014

Katika picha wakwanza kutoka kulia Raisi wa Rotary Club Orsterbay bwana Thomas Scherer, wapili kutoka kulia ni Mh. Shukuru Kawambwa , na wakwanza kutoka kushoto ni meneja kamati ya huduma ya Rotary Bi Sophia Mang'enya 3 

Wananchi wa kijiji cha kerege wamenufaika na huduma ya bure ya matibabu inayotolewa na klabu ya Rotary ya Oster Bay ya jijini Dar es Salaam kila mwaka katika shule ya msingi ya Kerege-Bagamoyo.

Akizungumza na wanahabari waliofika kujionea aina ya huduma za matibau zinazotolewa na klabu hiyo, Dk. Shukuru kawambwa,mbuge wa bagamoyo , Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi akiwa kama mgeni rasimi amesema kuwa amefurahishwa na kitendo hicho cha wanachama wa Rotary klabu na kuwataka wananchi wa Kerege wajitokeze kwa wingi siku nyingine kwani huduma hiyo ni bure.

“Ningependa kuwashukuru wanachama wa Rotary kwa msaada huu wa huduma ya matibabu ya bure kwa wakazi wa kerege na niwakuigwa katika jamii. Na pia ninawaomba wanakijiji wa kerege mjitokeze kwa wingi kwani huduma hii ni ya bure, unapima afya yako, unapata ushauri kutoka kwa madakitari bingwa mia moja”, Alisema Dk.Shukuru.

Naye Bwana Thomas Scherer ambeye ni raisi wa klabu hiyo amesema kuwa anajiskia furaha kuona wanachama wa klabu hiyo wakiwa na moyo wakijitolea kwa ajiri ya jamii inayowazunguka.

“Tuna furaha na tunajivunia ya kwamba kwa kupitia juhudi za pamoja za jamii, wanachama wa klabu za Rotary nchini na nje ya nchi, serikali za mitaa na taasisi, mashirika yasiyo ya kiserikali, jumuiya ya matabibu na sekta binafsi; tumeweza kuandaa Kambi hii ya matibabu kwa mara ya nne," alisema Thomas Scherer, Rais wa mwaka 2014-2015 wa Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oyster Bay.

Kambi ya Matibabu, sehemu mojawapo ya Miradi ya Afya ya Jamii, ambayo hufanyika kila mwaka toka ilipozinduliwa mwaka 2011 katika kitongoji cha Chanika jijini Dar es Salaam ambapo takribani wananchi 600 walijitokeza kupima malaria, VVU, kisukari, magonjwa ya mfumo wa upumuaji, macho na viashiria vya magonjwa sugu.

Pia Dawa za bure na miwani zilitolewa kwa watu waliokutwa na matatizo ya afya na macho. Mwaka 2012 tulitoa huduma kwa watu zaidi ya 700, na kutoa huduma kwa idadi kama hiyo katika mwaka 2013. Mwaka huu, inatarajiwa kuwa idadi hiyo hiyo ya watu watakaowahi kufika watasajiliwa ili kupata matibabu bure.
Posted by MROKI On Friday, November 21, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo