Nafasi Ya Matangazo

September 20, 2014

Na Fadher Kidevu Blog
MSHAMBULIAJI  raia wa Brazili Geilson Santana Santos JAJA jana ameshindwa kuingarisha tena timu yake ya Yanga baada ya jana kuambulia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Wanatamtam Mtibwa Sugar.

Katika mchezo huo uliokuwa wa ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2014/15 uliofanyika kwenye uwanja wa Jamuhuri Morogoro hadi mapumziko Mtibwa ilikuwa mbel kwa bao mja lililofungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba Mussa Hassani Mgosi kwa shuti kali dakika ya 15.

Kipindi cha pili Yanga walikianza kwa kasi na kupata penati lakini JAJA,alishindwa kuonyesha makali kama ilivyokuwa kwenye mechi ya Ngao ya Jamii Jumapili iliyopita baada ya mkwaju huo kupanguliwa na kipa wa Mtibwa Said Mohamed.

Bao la ushindi la vijana wa Mecky Mexime aliyewahi kufundisha na kocha wa Yanga Marcio Maximo, lilifungwa na Amme Ali dakika ya 82 na kuvunja matumaini ya Yanga kupata angalau sare katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali kwa pande zote mbili.

Kikosi cha Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Omega Seme, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite/Said Bahanuzi dk72, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Genilson Santana ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza/Simon Msuva dk46.

Mtibwa Sugar kilikuwa; Said Mohammed, Hassan Ramadhani, David Luhende/Majaliwa Shaaban dk64, Salim Mbonde, Andrew Vincent, Shaaban Nditi, Ali Shomary, Muzamil Yassin, Ame Ali, Mussa Mgosi/Vincent Barnabas dk50 na Mussa Nampaka/Dickson Daud dk72. 
Posted by MROKI On Saturday, September 20, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo