Nafasi Ya Matangazo

September 11, 2014

Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni 4.5/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Mwakilishi wa Afisa Elimu ya Sekondari Manispaa ya Temeke, Yasintha Kayoza kwa niaba ya shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Mbagala jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbagala, Mwalimu Marcelina Kimario.
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (mwenye miwani), akiangalia moja ya vitabu vya masomo ya sayansi baada ya kuvikabidhi vitabu vyenye thamani ya milioni 4.5/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Mbagala jijini Dar es Salaam jana.
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya milioni 1.5/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbagala, Mwalimu Marcelina Kimario katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam jana. Sekondari nyingine zilizokabidhiwa vitabu hivyo ni pamoja na Mvuti na Kambangwa. Kushoto ni Mwakilishi wa Shule ya Sekondari Kambangwa, Mwalimu Sueiba Mfinanga.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mbagala wakifurahia vitabu vya masomo ya sayansi, baada ya Kampuni ya Airtel kupitia Mradi wake wa ‘Shule Yetu’ kukabidhi vitabu hivyo vyenye thamani ya milioni 4.5/- kwa shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam jana.
*********
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa “shule yetu” umeendelea na mpango wake wa kuchangia katika kusaidia sekta ya elimu nchini ambapo leo imetoa msaada wa vitabu kwa shule 3 za sekondari jijini Dar es saalam

Shule zilizofaidika na msaada huo ni pamoja na Kambagwa sekondari iliyopo wilaya Kinondoni, shule ya sekondari Mvuti iliyopo wilaya ya Ilala na shule ya sekondari Mbagala iliyopo wilaya ya Temeke ambapo kila shule imepata vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano.

Akiongea wakati wa kukabithi vitabu hivyo, Meneja huduma kwa jamii Airtel Bi Hawa Bayumi alisema” Tunayofuraha kuendelea na mpango huu wa “shule yetu” kwa mwaka huu na kuwa na shule mpya zitakazofaidika na vitabu vya masomo ya Sayansi. Tunazo shule zaidi ya 30 ambazo tumezipata kwa kushirikiana na uongozi wa serikali zitakazofaidika na msaada huu wa vitabu kwa mwaka huu, Na leo tumeweza kuzifikia shule za Kambagwa, Mvuti na Mbagala na kuwapati vitabu vitakavyoweza kuleta tija katika ufaulu na elimu kwa ujumla”.

“Nia yetu ni kuendelea kushirikiana na Serikali chini ya wizara ya elimu katika kuinua sekta ya elimu nchini huku tukiwekea mkazo katika masomo ya sayansi kwani tuaamini ulimwengu na nchi inahitaji wanasayansi wengi ili kwenda na kasi ya ukuaji wa technologia. natoa wito kwa walimu na wanafunzi basi watumie vitabu vizuri na kuweza kuongeza wanafunzi wengi katika masomo ya sayansi na hatimae kuongeza ufaulu zaidi.aliongeza” Bayumi

Akiongea kwa niaba ya walimu wakuu wa shule zilizopokea msaada jijini Dar es saalam, Mwalimu mkuu wa shule ya Mbagala Bi Marcelina Kimaro alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa kutufikia leo, tumekuwa tukiona shule nyingi zikifaidiaka na mpango huu wa “Shule yetu” na leo tunayofuraha kupokea msaada wa vitabu vya Hisabati, Chemia, physikia na Baiologia kutoka Airtel

Shule hii ya mbagala Sekondari ina jumla ya wanafunzi 2031 na uwiano wa vitabu kwa wanafunzi kwa sasa ni kati ya kitabu kimoja kwa wanafunzi wa 3 au 4 , kwa msaada huu leo utasaidia kupunguza changamoto tuliyonayo ya uhaba wa vitabu na kufanya uwiano kuwa kitabu kimoja kwa wanafunzi wawili. Halikadhalika msaada huu utatupatia urahisi katika kusoma na walimu kuandaa masomo yao.

Kimaro aliongeza kwa kusema” Vitabu hivi vimetupa changamoto kubwa ya kuongeza juhudi katika masomo kwani nyenzo sasa tunazo na tunaamini wanafunzi wetu wa masomo ya sayansi watasoma kirahisi na hatimaye kupata idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi. Tunawaahidi kuvitunza na kuvitumia vitabu hivi kwa faida ya wanafunzi na jamii kwa ujumla”

Chini ya mpango wa “shule yetu” Airtel imeweza kutoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari zaidi ya 1000 nchini huku mpango ukiwa ni kizifikia shule nyingi zaidi kila mwaka.
Posted by MROKI On Thursday, September 11, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo