Nafasi Ya Matangazo

August 29, 2014



Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya baadhi ya Mawaziri waliohudhuria  mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi ulio wahusisha mawaziri wa mazingira na mawaziri wa mambo ya nchi za nje kutoka katika baadhi ya nchi za Afrika leo jijini Dar es salaam.
*****

Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda leo amefungua mkutano wa Mawaziri wa Afrika wa Mazingira na Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka katika baadhi ya nchi za Afrika jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo ambao ufunguzi wake uliongozwa na agenda kuu iliyozungumzia mwongozo wa namna ya kushughulikia changamoto zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabianchi, na ambavyo nchi zaAfrika zitakavyoweza kunufaika na rasilimali zinazotolewa na nchi zinazoendelea ili kukabiliana na jangahilo.

Aidha Waziri mkuu Pinda alielezea kuwa mkutano huo pia una umuhimu kwa nchi za bara la Afrika piautahusisha namna ambavyo serikali za Afrika zinaweza kukabiliana athari zitokanazo na mabadiliko yaTabiachi. Pia alisema kuwa mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya mkutano mkubwa wa mabadilikoya Tabianchi utakaofanyika mjini Newyork Marekani unaotegemewa kufunguliwa na Katibu Mkuu waUmoja wa Mataifa Bw. Baink Moon.

“Wote tunafahamu kwamba mabadiliko ya Tabianchi yanaathari kubwa kwa dunia nzima ila madharayake yanatofautiana kutokana na mabara, vizazi, umri, nafasi, matabaka pamoja na kipato” Aliongezakuwa kutokana na uchumi tegemezi wa nchi nyingi za Afrika nchi hizo zimekuwa zikiathirika zaidi
kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kiwango kidogo cha kuhimili athari zitokanazo na mabadilikoya Tabianchi na kuwa na uchumi mbovu.

Aliendelea kusema kuwa Afrika na Jamii za kimataifa zinatakiwa kuwa na utashi wa kisiasa katikakuungana kwa pamoja ili kuweza kushirikiana katika kupunguza uzalishaji wa gesi joto pia katika kuhimilina kukabiliana na athari hizo.

Mkutano huo wa Mabadiliko ya tabianchi uliofanyika leo jijini Dar-es-salaam umehusisha baadhi yaMawaziri wa Mazingira na Mawaziri wa Mambo ya nje ambao ni wajumbe wa kamati ya nchi za Afrika yaMabadikliko ya Tabianchi.
Posted by MROKI On Friday, August 29, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo