Nafasi Ya Matangazo

June 19, 2014


Mwandishi na mtangazaji wa habari wa siku nyingi, Bwana Edward Kahurananga, amefariki dunia hapo juzi tarehe  17/6/2014 baada ya kuugua na kulazwa kwa muda mfupi.

Marehemu Edward Kahurananga alizaliwa tarehe 25 Desemba, 1949 katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma. Alihitimu elimu ya Sekondari mwaka 1968 katika Sekondari ya Livingstone iliyoko mkoani Kigoma.

Katika uhai wake alisoma vyuo mbalimbali vya uandishi wa habari ndani na nje ya nchi. Mwaka 1970 aliajiriwa na Radio Tanzania Dar es Salaam kama Mtangazaji Msaidizi daraja la III. Alifanya kazi katika ngazi  mbalimbali katika mikoa katika mikoa kadhaa nchini chini ya Radio Tanzania Dar es Salaam .

Baadaye aliteuliwa kuwa  Mhariri wa Habari Mkuu wa Radio Tanzania Dar es Salaam kabla haijaunganishwa na Televisheni ya Taifa kuunda TvT ambayo baadaye ilibadilishwa kuwa TBC.  Mwaka 2004, Marehemu Edward Kahurananga alihamishiwa Idara ya Habari-MAELEZO kama Afisa Habari Mkuu.Wakati ule Idara ya Habari ilikuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.  

Tarehe 25 Desemba, 2009, Edward Kahurananga alistaafu kazi kwa mujibu wa kanuni za Utumishi wa Umma wakati huo Idara ikiwa imehamishiwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Edward Kahurananga alianza kuugua akiwa Mwanza na kulazwa katika hospitali ya Bugando lakini akahamishiwa hospitali ya Rufaa ya Muhimbili ambapo amefia tarehe 17 Juni, 2014 wakati wakiendelea kujaribu kuokoa maisha yake.Atazikwa kesho (Ijumaa) tarehe 20 Juni, 2014 nyumbani kwake Vikindu jijini Dar es Salaam.

MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMINA
Posted by MROKI On Thursday, June 19, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo