Nafasi Ya Matangazo

April 09, 2014

Na Mwandishi Wetu
Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang’anyiro cha kusaka malkia wa Tabata, Redds Miss Tabata 2014, watatambulishwa  siku ya sikukuu Pasaka katika ukumbi wa Da West Park, Tabata.
 
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema jana kuwa utambulisho huo utaenda sambamba na uzinduzi wa Miss Tabata 2014.
 
Kapinga alisema kuwa wapenzi wa urembo watapata fursa ya kuwaona warembo hao siku hiyo kabla ya kushiriki kwenye shindano la Redds Miss Tabata ambalo limepangwa kufanyika mwishoni wa mwezi ujao.
 
Katika uzinduzi huo warembo hao watasindikizwa na washiriki wenzao wa Miss Mzizima na Miss Ukonga.
 
Pia watakuepo viongozi waandamizi kutoka kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Hashim Lundenga na Redds Miss Tanzania Happiness Watimanywa.
 
Kapinga alisema washiriki 21 wanaendelea na mazoezi ya Miss Tabata kila siku katika ukumbi wa Da West Park chini ya wakufunzi watatu -  Neema Chaki, Pasilida Bandari na Bokilo.
 
Warembo hao ni Esther Frank Kiwambo (20), Jemima Huruma Mawole (22), Badra S. Karuta (20), Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22), Agnes Tarimo (18),  Agnes Alex (20), Catrina Lawrence Idfonsi (20), Nuru Omary Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).
 
Wengine ni Annatolia Raphael (21), Mary Henry (21),  Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail (20),  Ester Wilson Mbayi (20), Ambasia Lucy Mally (22), Faudhia Hamisi (21), Najma Charles Mareges (19), Lightnes Olomi (18), Husna Ibrahim (19) na Ramta Mkadara (20).
 
Warembo watano kutoka Tabata watashiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Miss Ilala baadaye mwaka huu.
 
Mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata ni  Noela Dorice Mollel ni Redds Miss Ilala.
Miss Tabata inaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.
Posted by MROKI On Wednesday, April 09, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo