Nafasi Ya Matangazo

December 18, 2013

Ndege ya abiria aina ya Boeing 767 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) ikiwa imesimama nje ya Uwanja wa Ndege wa Arusha baada ya kushindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutoka na hitilafu iliyokuwepo Uwanjani hapo na kulazimika kutua kwenye uwanja huo kwa dharula.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria zaidi ya 200 na wafanyakazi 9. kabla ya kupaa tena ilibidi abiria wote wateremke, na kupunguzwa mafuta ili kupunguza uzito wa ndege hiyo. Abiria waliamuriwa kwenda kupandia ndege hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA.
Tairi za ndege hiyo zikiwa zimejikita kwenye Udongo.
 
Hakuna anaeamini kama ndege hiyo imeweza kushuka uwanjani hapo.
Posted by MROKI On Wednesday, December 18, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo