Nafasi Ya Matangazo

September 24, 2013

 Mratibu  wa  maadhimisho ya  unywaji  wa maziwa mashuleni  Iringa  kutoka kampuni ya  Asas Bw Tony Adam katikati  akizungumza na  wanahabari Iringa  katika ofisi  za IPC juu ya maadhimisho hayo ,kulia ni katibu  wa chama cha  waandishi wa habari mkoa  wa Iringa Bw  Francis Godwin na kushoto ni afisa habari  wa kampuni ya maziwa ya  Asas
 Wanahabari  wa  vyombo mbali mbali  wakimsikiliza kwa makini mratibu  huyo

Na  Francis Godwin, Iringa 
WAKATI   kesho ni maadhimisho ya  siku ya  unywaji maziwa  duniani ,kampuni ya maziwa  ya  Asas Dairies Limited  Iringa inakusudia kuwanywesha  maziwa  wanafunzi 30,000  wa  shule  za msingi katika Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa kama  sehemu ya  kuhamasisha  jamii  kujenga  utamaduni wa kunywa maziwa kwa afya .

Akizungumza na wanahabari leo  katika ofisi za IPC ,mratibu  wa uhamasishaji unywaji maziwa  mashuleni  kutoka kampuni ya  ya maziwa  ya Asas Bw  Tony Adam  alisema  kuwa kuwa  wakati madhimisho  ya  unywaji maziwa kitaifa yanafanyika katika mkoa  wa  Tanga ,Kampuni  hiyo ya Asas Dairies Ltd  yenye makao  yake makuu mkoani  Iringa  imelazimika  kufanya maadhimisho  hayo mjini Iringa kwa kushirikiana na uongozi  wa Manispaa ya  Iringa.

Mratibu  huyo alisema  kuwa shule zote za Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  zitapata  kupewa maziwa katika  uwanja  wa  Samora   mbele ya mgeni rasmi  mkuu  wa mkoa wa  Iringa Dr Christine Ishengoma .

PIa alisema kuwa  wanafunzi  wote  wa shule  za msingi wenye  miaka chini ya 10 watashiriki katika mashindano  ya  uchoraji  wa  picha  za rangi  zitakazobeba  ujumbe  wa maziwa kwa  mfano  ng'ombe akila majani  ama  mtoto  akinywa  maziwa .

Mbali ya  watoto  kushindana  kuchora  pia  watu  wazima  watapata kushiriki semina  itakayoelezea  umuhimu  wa unywaji  wa maziwa na madhara  ya kutotumia maziwa katika  mwili  wa binadamu  na  kuwa  semina hiyo itahusisha  pia  wadau wa maziwa na viongozi  wa  mkoa  na Manispaa ya  Iringa pamoja na wawakilishi wa taasisi  zinazohusika na sekta ya maziwa za  zile bodi ya  maziwa , lishe na  chakula nchini (TFNC).

Alisema  madhumuni makubwa ya madhimisho hayo ni  kuamsha  hisia  za  wakazi  wa Manispaa ya Iringa  kuhusu umuhimu  wa unywaji maziwa  katika kujenga afya ya mwili  na kiakili zaidi.

Kwani  alisema  kuwa  kiwango cha unywaji  wa maziwa  nchini bado ni wa  kiwango  cha chini  sana cha  wastani  wa lita  40  za maziwa  kwa mtu  kwa  mwaka  ambazo zimepanda  lita  60 za maziwa kwa mtu kwa  mwaka  ikilinganishwa na kiwango  cha  kimataifa  (WHO) cha  lita 200 za maziwa  kwa  mtu kwa mwaka au  kiwango cha majirani zetu  Kenya  cha  lita 120 za maziwa kwa  mtu mmoja kwa  mwaka .

Alisema  kuwa kiwango  chetu hapa  nchini  ni sawa na na unywaji  wa maziwa  cha  pipa moja la maziwa  kwa mtu  mmoja kwa mwaka huku dhamira  ya kiwanda  cha Asas Iringa  ni  kuona  kiwango  hicho  kinaongezeka kufikia  lita  80 hadi 100 za maziwa  kwa mtu mmoja kwa  mwaka ndani  ya  kipindi cha miaka 5  ijayo.

Mratibu  huyo  alisema  kuwa kiwanda  hicho  cha  Asas Dairies  Ltd  kimeendelea  kufikisha  bidhaa zake kwa  wananchi  wengi zaidi nchini kwa  kuhakikisha wanafikiwa na huduma zao  na kutaja bidhaa zinazozalishwa  kuwa ni maziwa fresh,maziwa  mgando ,Yogurts zenye  ladha mbali mbali .

Aidha  ametaja  kaulu  mbio  ya  maadhimisho ya unywaji  wa maziwa mashuleni katika Manispaa ya  Iringa kwa mwaka  huu kuwa ni UNYWAJI  WA MAZIWA KILA SIKU SHULENI NI  HAKI YA  KILA MWANAFUNZI.
Posted by MROKI On Tuesday, September 24, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo