Nafasi Ya Matangazo

August 16, 2013

Wakati vita ya kupambana na wafanya biashara wa dawa za kulevya nchini Tanzania ikisha kasi kwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harison Mwakyembe kuweka bayana majina ya Wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JNIA walio husika katika zoezi la kufaulisha mabegi 9 yaliyo na dawa za kulevya kwenda Afrika Kusini,Abiria wa Tanzania akamatwa Hong Kong na heroin ikiwa ndani ya mashine
Waziri Mwakyembe aliwataja watu hao leo ambao ni maofisa usalama, Polisi na mbeba mizigo wa uwanja huo wa Ndege wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere.

Lakini hayo yakitokea nchini Tanzania kwa Waziri wa Uchukuzu kula kiapo cha wanaolidhalilisha jina la baba wa Taifa kupitisha madawa ya kulevya.

Kwa mara nyingine jana tarehe 15/8/2013, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa katikati ya chuma cha mashine.

Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za hongkong (167,500 us dollars)

Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.

Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni kifungo cha maisha na faini ya dola milioni 5 za hongkong.
Posted by MROKI On Friday, August 16, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo