Nafasi Ya Matangazo

August 29, 2013

Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia takriban dakika 25 zilizopita.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika  kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.

BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe. SOURCE: http://gospelkitaa.blogspot.com
Posted by MROKI On Thursday, August 29, 2013 2 comments

2 comments:

  1. to God be the glory,kazi ameimaliza ana haki ya kupumzika.

    ReplyDelete
  2. Kwakweli BWANA YESYU amemtwaa mtumishi wake kwa ulinzi mkali wa Malaika wa BWANA,ndivyo ninavyo aminikabisa.Alikuwa zawadi kwa Tanzania.Kwa hiyo tumeondokewa na zawadi mbili Kulola na Nyerere.Basi jina la BWANA litukuzwe,tuyafuate yale aliyokuwa akiyasema katika mikutano yake mikubwa ya Mnazi mmoja,Kidongo chekundu na Temeke EAGT-DVD zipo kwa anaetaka kuangalia na kusikia Injili yake mikoa ya Kusini,Ijumaa kuu-jumbe nzito.-Nnko documentary wa mikutano ya kulola ya Dsm 1996-2000.MUNGU ATUSAIDIE

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo